Sikubaliani na suala la kufuta sherehe za Nanenane mwaka huu 2021

Wafute na sherehe ya wafanyakazi na Sabasaba ili mzani uwe sawa.
 
Tumefuta nanenane badala yake tuwe na maonesho ya mitambo ya ketengenezea madaraja na ndege maana ndiyo vipaumbele vyetu.
 
Wangefuta mbio za mwenge maana ni upotevu wa pesa za mlipa kodi, lkn kufuta sherehe za Nanenane sidhani kama ni sahihi. Mkulima hajatendewa haki kabisa
Maambo ya ovyo yanayofanyika kwenye mbio za mwenge huchangia sana kueneza ukimwi.
 
Maonyesho huwa yanatusaidia mabo mengi sana afu eti mtu anakurupuka as if ni sherehe,nimewashangaa sana.Any way 20 tena
 
Yale maonyesho ni ya muhimu sana tofauti na wanavyofikiri, japo umeelezea kwa uchache lakini umegusa maeneo muhimu yaliyopaswa kuzingatiwa.

Wazo langu: Kama serikali kupitia wizara ya kilimo imeshindwa kuadhimisha hii sherehe pamoja na zile nyingne kama za Uhuru kwa kisingizio cha kutumia fedha husika kwenye maeneo mengine, kwa nini serikali isitafute wadhamini au waandaji wa hizi sherehe? Kwa mfano, waseme chama cha wakulima waandae sherehe hizi na wadhamini wakawa makampuni mbalimbali yanayojihusisha au yasiyojihusisha na kilimo au hata watu binafsi, kuliko mwaka upite bure kabisa while mkulima anatakiwa apatiwe siku yake kwa ajili ya kuonyesha kitu tofauti ndani ya sekta hii ya kilimo.
 
Una mawazo mazuri ila ni mawazo yako wewe mwenyewe kwa kifupi mkulu hawez kuyazingatia
 
Hivi haiwezekanani kinachofanyika 88 kufanyika 77 au vice versa? Kama nakumbuka vema, si zamani sana kuna kimojapo kati ya 77 na 88 hakikuwepo.
 
Ila siku hiyo ya 88 tunaruhusiwa kukusanyika maeneo ya 88 nakutafunatafuna vinyama vyambuzi? Nauliza
 
Nimepoteza fursa ya kujua kile ambacho nilidhamiria kwenda kujifunza kwenye sherehe za nane nane, pia ni sehemu ambayo huwa tunafanya ulinganifu wa mbegu ili kuijua ipi ni bora. Pamoja na yote inputs huwa tunanunua kwa unafuu kupitia mawakala ambao huwa wanapatika maeneo hayo.
 
Nchi inaendeshwa vile impendezavyo MTU mmoja yaani JoPoMa!! Akikumbuka daraja lakwao ndo tunajenga,akitaka ndege zitue kijijini kwao tunafanya,asipotaka katiba sisi hewalaa, mishahara ya watumishi niyeye aamue...kiufupi hakuna mambo ya kinchi ni kimhishmiwa anajiskiaje na anatakaje....
Waziri asilaumiwe maana huwa wanaambiwa tuu kuliaa-geuka... chapu unageuka hakuna kuhoji!!
Kimsingi tulikubali tulipokuwa waoga kudai katiba mpya sasa tuishi ujingani wajukuu wetu pengine wataondoa huu upuuzi nakulikomboa taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…