Ndugu zangu Watanzania,
Kwanza ningependa kuendelea kutoa pole kwa wana CHADEMA kwa kifo cha kiongozi wao.najuwa kibinadamu inaumiza , kusikitisha,kuhuzunisha na kutia simanzi.
Lakini ningependa kusema ya kuwa tukio hilo lisifanye kupoteza imani kwa vyombo vyetu vya Ulinzi hususan jeshi la Polisi kama ambavyo tumesikia matamko yakitolewa na viongozi na Makada wa CHADEMA.
Ni wazi kuwa jeshi letu limepokea na kusikia sauti za watanzania wa vyama vyote na wasio na vyama namna walivyo laani na kukemea tukio hilo na ndio maana tumeshuhudia likiongeza nguvu ya timu nzito kutoka makao makuu kitengo cha upelelezi wa matukio makubwa.
Tumeona pia namna Rais wetu Samia Suluhu Hasssan alivyosikitishwa na kuhuzunishwa sana na kutoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina na kupewa taarifa au ripoti juu ya suala hilo.
Lakini ningependa kusema kuwa unapokuwa kiongozi ni lazima na muhimu sana na busara kubwa sana kuchunga ulimi wako au maneno yako au kujizuia kuzungumza unapokuwa katika hali ya hasira,jazba au hali yoyote ile inayoweza kukufanya au kukuchochea kuzungumza jambo au kutoa tamko bila kufikiri zaidi ya kutumia hisia tu.
Ndio maana unapoitwa au kufikia hatua ya kuwa kiongozi ni lazima uwe na kifua,kujizuia kutanguliza hisia zaidi ,uchuje maneno,uwe na subira,utangulize hekima,busara na kuwa na Utulivu wakati wa nyakati ngumu zenye kila aina ya presha ya wafuasi wako au kwa sababu ya tukio fulani. Ni lazima uhakikishe ya kuwa unajizuia hisia zako katika kufanya maamuzi au kutoa maneno juu ya jambo fulani.
Sasa nimepita katika ukurasa wa Twitter wa Sugu mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa na kushangaa sana alicho kiandika. Kiukweli sikubaliani nacho kwa sababu kinaleta taharuki, uchochezi, uchonganishi na hofu kwa watu isiyo na ukweli. Ni maneno yanayoonyesha ameandika akiwa na hisia na kukosa utulivu au kufikiria kabla ya kuyaandika.
Kama kiongozi amekosea na amefanya kosa kubwa tu. Ameshindwa kujiongoza Mwenyewe na kutawala hisia zake na badala yake hisia zake zimemtawala na kumuongoza,jambo ambalo ni la hatari kwa kiongozi.Maana linakupunguzia ile nguvu ya kuitwa kiongozi Makini.
Maneno yenyewe na ujumbe wenyewe ni huu hapa.
PIA SOMA
Mara nyingi nikiangalia unaachoandika huku kwenye jukwaa huwa napuuza sababu kwa kiasi kikubwa huw aunaandika ngonjera za kufikirika na dhanania ambazo sio halisi ni zina kila namna ya kujikomba kwa wenye mamlaka ili kukidhi tamaa zako binafsi za kujulikana (umaarufu) au kupewa cheo kwa sababu mifumo iliyojengwa hivi karibuni ikianzia na JIWE inaruhusu hayo kufanyika kwa gharama za kutweza utu wa watu na wakati mwingine gharama za damu za watu.
Baada ya kupita humu jukwaani hasa kipindi hiki cha msiba mzito ambapo Mtanzania mwenzetu ameuawa kikatili baada ya kutekwa na baadaye mwili wake kutelekezwa Ununio, Ni matarajio yangu kwamba ungeingiwa na hofu na kuwakumbusha watu hasa wenye mamlaka ambayo wameitwaa kwa nguvu kukumbuka kuthamini uhai ambao ni zawadi tunayopewa na Mungu na sio kiumbe mwingine yoyote.
Nilitaraji ungeficha ujinga wako na ulikumbushe jeshi la polisi na idara ya usalama wa taifa ambayo Rais hivi karibuni ameitungia sheria ya kuruhusu kufanya ukamataji na kuwakinga watumishi wake dhidi ya mashtaka ya jinai ambayo ni kama haya yanayotokea. Nilitarajia ungetoa wito kufanyike reforms kwenye idara ya polisi hasa kwa namna inavyoshughulikia mambo kama haya na jinsi yanavyotokea katika jamii.
Kwanini Jongwe kaka yako kutoka Mwanjelwa amekua na uthubutu kwa kuandika ukweli huo aliouandika hapo:
1. Taarifa na malalamiko ya kuwa kuna watu wanapotea na kutekwa katika mazingira ya kutatanisha zilienea sana kwa kipindi hiki na majibu ya Mama yako ilikua kwamna ni drama na watu wanajiteka na sio kweli. Leo hii watu hawaonekani na mtu amekutwa amekufa.
2. Kule kanda ya ziwa kuna kiongozi mkubwa wa chama chako amenukuliwa na vyombo vya habari katika moja ya mikutano yake kwmaba wakosoaji wa ccm wakipotezwa polisi wasipoteze muda kuwatafuta (SIO POLISI HAO WALIOWAHI KUMUITA KUMHOJI AU CHAMA KUMCHUKULIA HATUA)
3. Sativa alitekwa na akaeleza mfululizo mzima akihusisha kituo cha Polisi Oysterbay, kupigwa risasi na hatimaye kutelekezwa katika pori huko katavi. Sio jalada la uchunguzi wala askari yoyote aliyewajibishwa isipokua serikali ilimpelekeafedha kugharimia matibabu what a shame! Ni kwa namna gani polisi wasihusike na matukio haya ya utekaji na mauaji?
4. Kijana Soka , ambaye alikua ni mkosoaji mashuhuru wa serikali anayeishi tabata akifcanya biashara ya Magari. Mpaka hivi sasa hakuna whereabouts zake na alikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa askari wa jeshi la polisi na walimfunga pingu huku wakimchukua na gari yenye namba za usajili la serikali. Polisi haijwahi kutoka kukanusha au kumshikilia mtu yeyote kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo linalojusu uhai wa Mtanzania ambaye hajafanya kosa la jinai je wasihusishwe na uharamia huo?
5. Mara kadhaa Masauni amenukuliwa na vyombo vya habari akikanusha juu ya utekaji na watu kupotea kwamba jambo hilo halipo na amekua akimtuma David Misime aongee kwa niaba yake na kufanya spining. Unachotakiwa kujua ni kwamba kuwa kwenye nafasi ya uongozi sio kwamba unajua au una ufahamu mkubwa sana kuliko wale unaowaongoza. Ni katiba yetu hii mbovu ndiyo inatruhusu wajinga kuongoza.
6. Bwana Mnyika aliarifu umma juu ya madhila ya kutoonekana kwa Mzee kibao, siku chache Misime anasema anasema polisi wanalifanyia kazi. Cha kusikitisha hakusema amefungua jalada la uchunguzi kituo gani, namba ya jalada au RB hakuna isipokua alitoa taarifa ya kuhadaa umma akijua wazikabisa anadanganya na umauti lazima utamfika mhusika. Je Jeshi la polisi lisihusike?
7. Mazingira ya kutekwa Mzee Kibao yanahusisha moja kwa moja jeshi la Polisi. Kama wewe hujawahi kufika Tegeta nearby Kibo Complex area ni sehemuambayo iko busy muda wote. Katika mazingira hayo alikuwepo Traffic police akiongoza magari, magari yakzuia basi mbele yake, watekaji wakapanda ndani ya basi wakiwa na silaha na kumkamata Mhusika huku wakiendelea kujitambulisha kama askari polisi. Wakashuka na mhusika na kuondoka nae kueleka wanakojua. Kama sio askari polisi traffic lazima angewataarifu watu watu wa patrol na wangefanya intervention ili kumnusurui Marehemu lakini hakuna chochote kilichofanyika. Je tuwatenge polisi na mfululizo wa mauaji hayo na utekaji?
8. Ndugu yenu huko aliyechoma picha inayosadikika ni ya Rais alikamatwa kwa ultimatum akapandishwa kizimbani na kuhukumiwa kwa muda mfupi. Baada ya kulipa faini ameachiwa huru lakini uhuru wake umepokwa na hajulikani alipo mpaka sasa. Jeshi la polisi licha ya kutuhumiwa lipo kimya hata kutoka kujisafisha .
9. Sijui i unafiki au ni utashi wa kweli, kikao cha chama kule Dodoma ambacho mnakiita bunge kilipoketi hivi karibuni. Mooja wa wajumbe aliomba kujadiliwe kwa hali hii lakini dada yako amabaye nae amewahi kuja na kauli "pita nae" akimaanisha kuwaua wakosoaji wa Kiongozi mwenzie akalitupilia mbali aksema sio wakati wake, labda ilikua ni drama.
nimalize: Ikiwa jeshi la polisi halihusiki, kwanini lisianzishe operesheni maalumu ya kukitafuta hiki kikundi cha kigaidi kinachotejka wananchi mfululizo na kuwaua? Kama jeshi la polisi halihusiki kwanini Hata Pale mwananyamala lilitaka kuzuia mwili wa Mzee unapofanyiwa postmetrm wanshaeria wa chama husika wasiwepo?
Lucas tetea ujinga wote wa Chama chako lakini sio kumwaga damu ya Mtu. Jongwe is right and will be right