ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,476
WanaJamii Sikubali kabisa na serikali yetu kwamba Pesa za ziada za ununuzi wa rada zirudi Serikalini ( HAZINA)
Jana nimemsikiliza Waziri wetu Membe akihojiwa na Charles Hilary wa BBC kuhusu pesa za zaida ambazo serikali ililipia katika ununzi wa Rada. Waziri anasema serikali ya Uingeleza lazima irudishe pesa hizi Hazina kwa sababu ni mali ya walipa kodi wa Tanzania.
"Lazima pesa hizi zirudishwe serikalini - HAZINA maana ni mali ya walipakodi na si vinginevyo, pamoja na mambo mengine pia nimekuja kufuatilia jambo hili kuhakikisha hawa wenzetu wanatuelewa" - Membe akiwa U.K.
Wakuu mimi sikubaliani kabisa na waziri kwa misingi ifuatayo
i) Baada ya fununu kuwapo na harufu ya rushwa katika sakata hili - je serikali ilifanya uchunguzi wowote?
ii) Na kama uchunguzi ulifanyika je serikali ilichukua hatua gani pamoja ya kuwafikisha wale wote waliohusika kufikishwa katika vyombo vya dola na sheria?
iii) Baada ya kusikia habari kuwa Serikali ya uingeleza inaanza kuchunguza sakata zima je serikali ilitoa mchango kamilifu?
iv) Je Serikali mpaka sasa imechukua hatua gani katika sakata hili baada ya kupata riporti kwamba kulikuwa na rushwa katika ununuzi na ushahidi kutolewa? na kama bado kivipi basi inakuwa nyepesi (serikali) kuomba pesa ambazo kwanza haikuwa na uchungu nazo zirudi serikalini?
Binafsi sina imani kabisa kwamba endapo pesa hizi ( 28,000 pounds) zikirudi Hazina zitakuwa salama, nina wasiwasi zisije zikaelekezwa kwenye matumizi mengine kama kampeni au hata kuyeyuka tu.Ninachoomba serikali iwaachie wale waliotusadia kuzikomboa hizi pesa waamue watazielekeza wapi kama aibu na tushaonekana ni watu wa aina gani mbele ya mataifa.
Wakuu nisaidieni hapa hii senario: Unaibiwa kitu then mtu anakwambia umeibiwa humjali - mtu huyo huyo anafanya uchunguzi na kukusaidia kupatikana kwa kitu chako na ushahidi anakupa kwamba furani ndiye mwizi au tapeli wako sasa badala ya kuanza kuhangaika na mwizi au tapeli wako wewe unataka jamaa akurudishie kitu chako kwanza - hapa sipati picha sababu watuhumiwa wapo mtaani tu wanakula kuku na wanajiandaa na uchanguzi mkuu majimboni kwao. kweli bongo tabararee
Binafsi nashauri hizi pesa zielekezwe kwenye wilaya zisaidie kuboresha zahanati hasa vitengo vya uzazi - Pesa hizi wapewe NGO's ili kufanya shughuli hii kwa usahihi na uwazi.