Sikukuu ya kesho itakuwa nzuri sana!

hawa wahenga nao wazinguaji tu hvi kwann walifananisha sindano ile ndogo na Mnyama mkubwa kias kile.?
wakati wangeweza kusema hata m'mbu tu,walienda mbali sana as if kuna mnyama wakupenya kwenye hilo tundu la sindano.
 
Ahahaha kula mwenyewe n uchoyo huo,,,,,,,,,,mualiko ulikuepo sema t umeniwahi.


Karibuni wanna JF wote tusherehekee pamoja.
Ha ha ha shukrani sana, tupe na location ya eneo ili tuanze kuandaa ndizi na pilipili za mwendokasi
 
Na mimi jamani nijumuike kufinya hilo pilau..tusitengane jaman..Dodoma si hapo tu?
[emoji4][emoji4]hapana ni kule
Umeshahesabiwa Kwanza [emoji848]

Anyway u a most welcome.
 
Si kweli, watu walipanga. Ilikuwa tarehe ya ibada ya kipagani watu wakaamua iwe ya kuzaliwa Yesu. Kwenye maandiko hakuna tarehe yoyote aliyozaliwa Yesu na wala hakuna agizo la kusherehekea kuzaliwa kwake.

Ila, tunaambiwa alizaliwa ili tuokolewe kwa dhambi zetu, si kula na kunywa au kufanya dhambi! Na ndiyo sababu ya Jina la Yesu kumaanisha atakayetuokoa na dhambi zetu.
Ni kweli alizaliwa 25/12/ au ni fix?
 
Kwa Wayahudi enzi hizo haikumaanisha sindano unayoijua leo. Kwanza haikuwepo! Kwao ilimaanisha lango dogo (eye of a needle) baada ya lango kubwa la mji kufungwa jioni au ukifika usiku.

Kwa waliochelewa kuingia kupitia lango kubwa walilazimika kuwapitisha ngamia wao kwenye lango dogo kwa taabu sana. Waliwalazimisha kujikunja miguu na "kushuka chini kabisa" kisha waliwatua mizigo yao ili wapenye kirahisi lango dogo na kuingia ndani.

Kushuka chini kwa ngamia ni ishara ya kunyenyekea au kutubu, na mizigo ni mali tunazoziabudu badala ya Mungu au dhambi zetu zinazotusonga sana. Wengi tukitajirika hatuko tayari kugawa mali zetu na kuwapa maskini au kuachana nazo kama si halali. Zaidi sana tutatamba nazo na hata kutamani kuwapora maskini. Hapo si rahisi kumfuata Yesu na/au kumpenda Mungu kwa dhati toka moyoni.

Na ikumbukwe kuwa zamani miji ilizungushiwa ukuta kama tunavyozungushia nyumba zetu sasa.
hawa wahenga nao wazinguaji tu hvi kwann walifananisha sindano ile ndogo na Mnyama mkubwa kias kile.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…