Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China yachochea uchumi wa dunia

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China yachochea uchumi wa dunia

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China yachochea uchumi wa dunia

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ni sikukuu kubwa zaidi ya Wachina, na inaweza kuchukuliwa kama kipimo cha uchumi wa China. Licha ya hayo, katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya China, sikukuu hiyo pia imekuwa kichocheo kikubwa cha wa uchumi wa dunia nzima.

Katika sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa mwaka huu, , Wachina wengi wamesafiri nje ya nchi, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeo la siku za mapumziko, ongezeko la nchi zisizohitaji visa kwa raia wa China, na kupungua kwa nauli ya ndege. Takwimu zinaonesha kuwa, idadi ya tikiti za ndege zilizoagizwa za kwenda nchi za nje kutoka China kati ya Januari 28 hadi Februari 4 ilizidi milioni 2, ambalo ni ongezeko la asilimia 21 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

Mwaka huu katika sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Wachina wametalii katika miji 2,100 ya nchi za nje duniani. Tovuti ya utalii ya Marekani inayoitwa Dunia ya Safari na Utalii iliripoti kwamba, wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China mwaka huu, idadi ya watalii wa China itavunja rekodi katika historia, na kuashiria kufufuka kwa soko la utalii duniani.

Katika sikukuu hiyo, wageni wa nchi mbalimbali pia wametalii nchini China ili kushuhudia utamaduni maalumu wa Kichina. Mwezi Desemba mwaka jana, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Umoja wa Mataifa (UNESCO) iliamua kuorodhesha Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye Orodha ya Urithi wa Kitamaduni Usioshikika wa Binadamu, jambo ambalo limeongeza umaarufu wa Sikukuu hiyo duniani.

Takwimu zinaonesha kuwa, wastani wa idadi ya watu walioingia na waliotoka forodha ya China kwa siku wakati wa sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ya mwaka huu ilifikia milioni 1.85, ambalo ni ongezeko la asilimia 9.5 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Ikiwa sikukuu muhimu zaidi ya Wachina, Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China sio tu sikukuu ya kukutana kwa familia, bali pia ni msimu wa kilele wa manunuzi. Kutokana na China kufungua mlango zaidi kwa bidhaa za nchi za nje, na kupunguza ushuru wa forodha, bidhaa za nchi mbalimbali zikiwemo cherries za Chile, kamba za Australia, zabibu za Afrika Kusini, na parachichi za Kenya zimechukuliwa na Wachina kama zawadi za Mwaka Mpya. Mwaka 2024, thamani ya bidhaa za nchi za nje zilizoagizwa ilivunja rekodi tena, na China inatarajiwa kuendelea kuwa soko kubwa la pili duniani kwa miaka 16 mfululizo.

Uchumi wa China hauwezi kutengana na dunia, na uchumi wa dunia pia hauwezi kuendelea bila ya China. Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China inachochea uchumi wa dunia, na hali hii imeonesha nguvu ya uchumi wa China, na pia imeonesha uhusiano wa karibu kati ya uchumi wa China na uchumi wa dunia.
 
Back
Top Bottom