Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SIKUMFAHAMU MAREHEMU MWALIMU ZUBERI WAZIRI NYUNDO LAKINI ATAISHI NDANI YA MOYO WANGU
Kwa kawaida taazia haijibiwi.
Ukishamaliza kusoma unamtakia maghufira marehemu.
Nimesoma taazia aliyoandika Ahmada Kidege baada ya kifo cha Zuberi Waziri Nyundo mwalimu mstaafu aliyekuwa akifundisha shule moja kijiji cha Negero Wilaya ya Kilindi.
Marehemu Zuberi Waziri Nyundo alikuwa mahabusu Jela ya Maweni kwa miaka mitatu kwa tuhuma za ugaidi.
Hapo Maweni ndipo Ahmada na Mwalimu Zuberi walipokutana na wote wakiwa watuhumiwa wa ugaidi.
Kwa mapenzi makubwa sana Ahmada anamwita Mwalimu Zuberi baba.
Kilichowakutanisha hawa Waislamu wawili si kingine ila msikiti uliokuwapo hapo jela.
Naomba nisimame hapa.
Kuna vitu vitatu vinazunguka akilini kwangu.
Kitu cha kwanza ni hili jina la Negero, kisha ugaidi na tatu ni hii taaluma ya usomeshaji ambayo watu hawa wawili wanayo.
Huu ualimu umekuwa ‘’kama common denominator’’ katika hawa Waislam wanaokamatwa kwa tuhuma za ugaidi.
Kuna kisa kama hiki cha hawa wawili waliokuwa mahabusu Maweni.
Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso yeye pia alikamatwa kwa tuhuma za ugaidi na akawekwa mahabusu.
Sheikh Chambuso ni mwalimu.
Kuna Athmani Khalfani Mrindoko.
Yeye ni mwalimu pia kama hawa wenzake.
Mwalimu Mrindoko kama wenzake alikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa shutuma za za ugaidi.
Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kijiji cha Lwande, Kilindi.
Kijiji hiki na kijiji kingine Madina jirani na Negero vilishambuliwa mwaka wa 2013 kwa tuhuma za ugaidi ikielezwa kuwa Al Shabab wapo katika vijiji hivyo na wana silaha za kutungulia ndege.
Shutuma hii haikuweza kuthibitishwa.
Lakini ukweli ulikuja kufahamika baadae kuwa hapakuwa na Al Shabab wala hapakuwa na silaha za kutungulia ndege.
Ikiwa ukweli ni huu nini kilichomponza Mwalimu Athmani Mrindoko hadi akamatwe kwa shutuma za ugaidi?
Haya yalitokea Lwande Wilaya ya Kilindi.
Kitu cha kwanza ni kuwa Mwalimu Athmani alikuwa mwalimu mwajiriwa na serikali kusomesha masomo ya kisekula lakini alijitoea kusomesha somo la dini kwa wanafunzi Waislam.
Siku za nyuma Mwalimu Athmani alifatwa na walimu wenzake akaelezwa kuwa imetoka amri juu kuwa walimu washirikiane kuwafaulisha watoto darasa la saba kwa kuwakokotolea wanafunzi majibu ya mtihani wa mwisho wa darasa la saba ili kunyanyua ufaulu wa shule na hatimaye wilaya.
Mwalimu Athmani akakataa hili kwa misingi ya Uislam kuwa huo ni udanganyifu na kitendo hicho hakitamnufaisha yeyote si wanafunzi shule au nchi kwa ujumla.
Sasa lilipotokea sakata la Lwande askari waliovamia kijiji kwa madai ya kupambana na Al Shabab Mwalimu Athmani akakamatwa, kupigwa na kufunguliwa kesi ya kujeruhi Mahakama ya Handeni.
Kijiji hiki cha Lwande kipo Wilaya ya Kilindi.
Marehemu Zuberi Waziri Nyundo aliyefariki hivi karibuni alikuwa mwalimu kama alivyokuwa Mwalimu Athmani Mrindoko na yeye alikuwa kutoka kijiji cha Negero, Kilindi.
Katika operesheni hii ya kupambana na Al Shabab Ijumaa moja wakati Waislam wako katika msikiti wa Ijumaa wa Madina katika sala, msikiti ulivamiwa na Waislam wawili Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir wakauawa kwa kupigwa risasi.
Msikiti na nyumba za Waislam zikachomwa moto.
Mkasa huu unastahili Makala maalum kueleza kwani ni kisa cha kuzuhunisha sana.
Juu ya haya yote haukupatikana ushahidi wowote wa silaha za kutungulia ndege wala kuwapo kwa Al Shabab kijijini hapo.
Akili ya kawaida tu itakuambia kuwa silaha za kutungulia ndege zitapita wapi kwenda Madina?
Kijiji cha Madina kipo Wilaya ya Kilindi.
Wakati haya yanafanyika habari zilifika Dar es Salaam na kusambaa katika barza za kahawa nje ya misikiti mingi kuwa Waislam wanauliwa sehemu za Tanga na kuna msako wa nyumba kwa nyumba Waislam wanakamatwa usiku wa manane.
Ilikuwa katika hali hii ndipo nikatembelewa siku moja na kijana mmoja akaniambia kuwa ana taarifa za kusikitisha kutoka Handeni na vijiji vya jirani ambako Waislam wameuawa na misikiti imechomwa moto.
Akanieleza kuwa Waislam wamemwagiza aje kwangu anifahamishe na kuniomba mimi nifikishe habari hizo kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje.
Nilimuuliza kama ana ushahidi wa hayo anayonieleza.
Aliniambia hana ushahidi wala asingethubutu kutafuta ushahidi kwani yeye anatoka Handeni na magari yote kuingia na kutoka; na njiani kuna upekuzi mkali khasa wakikujua kuwa wewe ni Muislam.
Mabasi yanasimamishwa na yeyote mwenye muonekano wa kuwa Muislam anashhushwa.
Akaniambia kuwa wanawake wanavua hijab na wanaume wananyoa ndevu na hawavai kanzu wala kofia kwa hofu iliyopo huko na hata darsa zilizokuwapo katika baadhi ya msikiti zimesimamishwa.
Waislam wakishasali wanaondoka kurejea majumbani kwao na misikiti inafungwa.
Nilimuomba turekodi mazungumzo yetu lakini akakataa.
Nikamuomba nimpige picha vilevile akakataa.
Lakini baada ya kuzoeana alinikubalia nimpige picha ila sura yake isitokee.
Huyu kijana alikuwa akija kwangu kwa takriban juma zima tunaungumza na mimi nachukua maelezo yake kiasi nikapata picha kamili ya yote yaliyotokea Kilindi.
Nikampa jina huyu kijana nikamwita Sheikh ‘’Deep Throat,’’ sawa na jina la yule mpashaji habari aliyetoa taarifa za kashfa ya Watergate.
Niliposoma taazia ya marehemu Zuberi Waziri Nyundo ikawa imenikumbusha mengi yanayowasibu Waislam nikaona hii ni fursa yetu kujikumbusha historia yetu.
Kijiji cha Madina, Negero hivi sasa ni mahame hakuna tena makazi ya watu.
Sababu ya kuwa hivyo ni kule kuhusishwa na Al Shabab.
Sasa inakaribia miaka tisa ushahidi bado haujapatikana hadi leo kama Al Shabab walipata hata kutia mguu katika ardhi hiyo achilia mbali kuwepo kwa silaha za kutungulia ndege.
Sikupata kumfahamu Mwalimu Zuberi Waziri Nyundo lakini siku zote ataishi ndani ya moyo wangu.
Niliweza kufika Handeni kimya kimya na nilifanikiwa kukusanya taarifa nyingi kwa yale yaliyotokea kwa picha na sauti.
Niiwafikishia marafiki zangu wengi ndani na nje ya nchi.
Ajabu ni kuwa wote waliniambia kuwa ushahidi umejitosheleza sana lakini kama vile walikuwa wameagana walinishauri tuliache suala hili.
Rafiki yangu mmoja katika vyombo vya habari vya kimataifa yeye alikwenda mbele zaidi ya wenzake akaniambia, ''Mohamed lipe muda hili suala iko siku In Shaa Allah utaandika kitabu kizuri sana.''
Mwenyezi Mungu Hakimu Muadilifu lipanue kaburi la huyu mja wako na lijaze nuru.
Amin.
PICHA: Sheikh ''Deep Throat,'' Athmani Khalfan Mrindoko, Rajab Ramadhani Chambuso kushoto na Ahmada Kidege, moja ya nyumba iliyochomwa moto Madina.