Dhambi zenyewe tunaambiwa zinaletwa na Shetani lakini hukumu Inakuja kwetuKama sijawahi kuomba kuletwa duniani, kuna haki gani ya kimantiki ya kunihukumu na adhabu ya moto wa milele?
Kama sijawahi kuomba kuletwa duniani, kuna haki gani ya kimantiki ya kunihukumu na adhabu ya moto wa milele?
Ujumbe wa Mada:
Kuja duniani haikuwa ombi, mkataba, wala uchaguzi wako wa aina yoyote. Hujaweka saini mahali popote, wala hukuchagua DNA yako, ubongo wako, wazazi wako, au mazingira uliyozaliwa nayo. Maamuzi ya kuingia kwenye huu ulimwengu yalifanywa na watu wengine bila ridhaa yako.
Pamoja na kutokuomba kuja hapa, unajikuta umetupwa katikati ya ulimwengu uliojaa changamoto tele, udhaifu wa kibinadamu, magonjwa, na mifumo magumu ya kiuchumi na kijamii ambayo hukuipangilia.
Huu ni mchezo ambao hukuchagua kushiriki, lakini papo hapo unalazimika kuucheza chini ya sheria ngumu sana
Jambo linaloibua mjadala ni muundo wa adhabu inayosemwa inamrejea binadamu baada ya kifo, Katika mfumo wowote wa haki na uadilifu adhabu inatakiwa ilingane na kosa husika, Inakuaje kosa au uasi uliofanywa ndani ya maisha mafupi sana ya miaka 60 au 80 ya binadamu aliyejaa udhaifu, upewe adhabu ya mateso yasiyo na mwisho?
Kimantiki, hii inavuka mipaka ya haki na kuelekea kwenye adhabu isiyo na kipimo, ambayo haina hata fursa ya kumrekebisha mhusika kwa sababu haina mwisho.
Pia, binadamu tayari anapitia dhiki, msongo wa mawazo, na changamoto nyingi wakati wa maisha yake ya hapa duniani. Kama kuna adhabu inatakiwa kuwepo, mantiki ya haki inasema adhabu hiyo walistahili kupewa wale waliokusababisha ukaja hapa na kushindwa kukupa misingi au mazingira bora ya kukukinga na kufeli, kuliko kumwadhibu kiumbe aliyeletwa kwa nguvu kwenye dunia hii yenye dhuluma.
Kumhukumu mtoto aliyetupwa kwenye uwanja wa vita bila zana badala ya waliomleta humo ni ukatili na roho mbaya.
Kama hukuomba kuja duniani, hukupewa fursa ya kuchagua zana wala mazingira ya kuanzia, kwanini uwajibikaji wako kwenye maisha haya ufuatiwe na vitisho vya adhabu kubwa kiasi hiki pale unapoteleza.
DuuuhUkweli kwamba hukuchagua kuzaliwa hauondoi moja kwa moja wajibu wa maamuzi unayofanya baada ya kuwa na uwezo wa kutambua mema na mabaya. Mtoto hawezi kuwajibishwa kwa hali aliyoikuta, lakini mtu mzima anaweza kuwajibishwa kwa matendo anayochagua.
kutokuchagua kuingia duniani na kutokuchagua chochote maishani.
Hata kama hukuchagua kuzaliwa, baada ya kuzaliwa unapata kiwango fulani cha uchaguzi. Ndiyo maana mifumo ya sheria haitoi msamaha wa kila kosa kwa sababu tu mtu hakuchagua kuzaliwa.
Kuna makosa ambayo tendo lenyewe linaweza kuchukua sekunde chache lakini madhara yake yakawa makubwa na ya kudumu. Kwa hiyo, urefu wa tendo pekee hauwezi kuamua uzito wa adhabu.
Hoja kuhusu adhabu ya milele inahitaji kwanza kuthibitisha kwamba mafundisho hayo yana maana hiyo. Huwezi kuanza kwa kudhani kwamba Ukristo unafundisha mateso yasiyo na mwisho kwa kila mtu anayekosea, halafu ukatumia dhana hiyo kuonyesha kwamba Mungu si mwenye haki. Hapo unahitaji kwanza kujadili tafsiri za Biblia kuhusu hukumu, jehanamu, uzima wa milele na wokovu.
Wazazi ndio wawajibike kwa kukuletea duniani.
Kama mzazi akizaa mtoto katika mazingira magumu, hilo linaweza kuwa jambo la kulaumiwa kimaadili katika mazingira fulani, lakini mtoto anapokuwa mtu mzima, hawezi kuhamisha kila jukumu lake kwa wazazi wake. Vinginevyo hakuna mwanadamu ambaye angekuwa na uwajibikaji binafsi.
Mfano wa mtoto aliyepelekwa vitani haujitoshelezi.
Mtoto hana uwezo wa kuchagua vita wala kujilinda. Lakini mtu mzima anayefanya uamuzi wa kimaadili akiwa na ufahamu ni hali tofauti kabisa. Mfano huo unatakiwa kutenganisha vizuri kutokuwa na uwezo wa kuchagua na kuwa na uwezo wa kuchagua lakini kuchagua vibaya.
Hakuna Mungu wala moto wa milele mkuu.Kama sijawahi kuomba kuletwa duniani, kuna haki gani ya kimantiki ya kunihukumu na adhabu ya moto wa milele?
Ujumbe wa Mada:
Kuja duniani haikuwa ombi, mkataba, wala uchaguzi wako wa aina yoyote. Hujaweka saini mahali popote, wala hukuchagua DNA yako, ubongo wako, wazazi wako, au mazingira uliyozaliwa nayo. Maamuzi ya kuingia kwenye huu ulimwengu yalifanywa na watu wengine bila ridhaa yako.
Pamoja na kutokuomba kuja hapa, unajikuta umetupwa katikati ya ulimwengu uliojaa changamoto tele, udhaifu wa kibinadamu, magonjwa, na mifumo magumu ya kiuchumi na kijamii ambayo hukuipangilia.
Huu ni mchezo ambao hukuchagua kushiriki, lakini papo hapo unalazimika kuucheza chini ya sheria ngumu sana
Jambo linaloibua mjadala ni muundo wa adhabu inayosemwa inamrejea binadamu baada ya kifo, Katika mfumo wowote wa haki na uadilifu adhabu inatakiwa ilingane na kosa husika, Inakuaje kosa au uasi uliofanywa ndani ya maisha mafupi sana ya miaka 60 au 80 ya binadamu aliyejaa udhaifu, upewe adhabu ya mateso yasiyo na mwisho?
Kimantiki, hii inavuka mipaka ya haki na kuelekea kwenye adhabu isiyo na kipimo, ambayo haina hata fursa ya kumrekebisha mhusika kwa sababu haina mwisho.
Pia, binadamu tayari anapitia dhiki, msongo wa mawazo, na changamoto nyingi wakati wa maisha yake ya hapa duniani. Kama kuna adhabu inatakiwa kuwepo, mantiki ya haki inasema adhabu hiyo walistahili kupewa wale waliokusababisha ukaja hapa na kushindwa kukupa misingi au mazingira bora ya kukukinga na kufeli, kuliko kumwadhibu kiumbe aliyeletwa kwa nguvu kwenye dunia hii yenye dhuluma.
Kumhukumu mtoto aliyetupwa kwenye uwanja wa vita bila zana badala ya waliomleta humo ni ukatili na roho mbaya.
Kama hukuomba kuja duniani, hukupewa fursa ya kuchagua zana wala mazingira ya kuanzia, kwanini uwajibikaji wako kwenye maisha haya ufuatiwe na vitisho vya adhabu kubwa kiasi hiki pale unapoteleza.
Sahihi hata Shetani hayupo, ni misemo Tu ya wajaHakuna Mungu wala moto wa milele mkuu.
Tunaunguzwa na moto wa jua hapahapa duniani tu ๐
Haya ndio majibu yanawafaa watu kama hao.Hakuna atakayekupa jibu sahihi humu. Kama vipi mtafute muhusika aliyekuleta duniani, akakupangia masharti ambapo ukishindwa unachomwa moto.
Naona mnafarijiana,๐Sahihi hata Shetani hayupo, ni misemo Tu ya waja
Thatโs a belief, not an established fact.Death is the ๐, there is no hell or heaven, when you die you cease to be, to exist, like before you were born