sikuomba kuzaliwa, kwanini nihukumiwe na moto wa milele

Kuzaliwa uliomba
Muda wa kuishi duniani uliomba pia
Siku ya hukumu utaonyeshwa documents zako ulizo Saini

Kama ambavyo Leo hii haukumbuki kilichokuwa kinakufarahisha ulipokuwa tumboni Kwa mama yako Hadi ukawa unafurahi na kuruka ruka ukiwa tumboni vivyo hivyo hauwezi kukumbuka ulipo Saini hizo documents za kuomba kuja duniani

Lakini pia Mungu alijua kuwa umesahau Kwa sababu ulikuwa katika ulimwengu mwingine ndio maana amekukumbusha Kwa kukuletea manabii na vitabu

Yani kichaka Cha kujificha hakitakuwepo
 
Hakuna Moto wa jehanam.
Ukifa umekufa hakuna lolote jipya.
Mengine kutishana tu ili tufuate miongozo flani ya kuishi na wengine duniani.
 
Watu wengi tu hawaamini kwamba Mungu atatuchoma milele...

Unaweza kuzungumza nao.

Nahisi wakristo kibao tu, waislamu sijui. Hivi wakatoliki wanaamini vipi kuhusu suala la motoni?
 
Mkuu kwani maisha yanaanza tumboni kwa Mama au kwa Baba, kwani bila Baba mama anaweza kupata mtoto

Naamaanisha sio kwamba bila Baba, wengi hii miili yetu si ingekuwa chooni kama bleed (hedhi)
 
Wakati wenzako wanachagua kwenda mbinguni wewe ulikuwa wapi?
 
Kuna muda utafika utajua there's no point of all these things... Ukifa ndio mwisho wako...

Na hakuna kitu ulicho ambiwa kuhusu wewe ni sahihi...

So ni either uishi kwa furaha kujua hakuna maana, au kwa huzuni kwa sababu hakuna maana
 
mkuu huko ulikokuwa kabla hujazaliwa hapa ulitenda dhambi sana, na utaendelea kuzaliwa kwenye huu ulimwengu mpaka unyooke.
 
Mala ooh FB nilishaifuta miaka mingi iliyopita.

Anyway tenda mema kwa kuuza mali zako zote uwapatie masikini... vipi kama ukikuta haya niya kweli.

Vipi ukienda mbinguni ukaambiwa freemason ilikuwapo kwajili ya kusaidia masikini

Yaani havieleweki wewe ishi tu vile roho yako inasema
 
Mtu anaamka anajikuta kwenye bonge moja la kasri lina kila aina ya anasa:

mavyakula, mavinywaji, ma swimming pool, magari, wanyama, ma video games, ma studio, wasichana warembo kawakuta humo...

Anaanza kutumbua non stop, anaonja kila kitu, kila kitu anaweka mkono wake, anavuruga kila kitu.

Baadae baada ya kulala na kila msichana, baada ya kula kila chakula, kila kinywaji, kujaribu kila alichokiona,

Huku nyumba imekuwa chafu, vitu vingine kaharibu, wasichana wanalia non stop wanamkera na vilio vyao wengine wamezaa na kuzaa, kala kanenepeana anaumwa, kanywa kazibuka kaisha,

Muda wote hajiulizi hili jumba la nani, vitu vya nani, kwanini niko hapa, hao wasichana aliowaona hapo nao wametokea wapi na kwanini wako hapo,

Ghafla bin vu kwa mbali wanaona msafara unakuja, huyo mwenye jumba kaja.

Nyumba yake ni chafu. Watoto wake wanalia. Vitu vimeharibika. Jamaa mwenyewe yuko hoi bin taabani kwa sonona na magonjwa,

Faza house anamwambia naomba niandikie ukurasa mmoja unielezee kilichotokea humu ndani.

Ndo hii thread yako.
 
Utawajibika kwa ulivyoishi maisha yako kwasababu utashi huo unao.

"Sikuomba kuletwa" sio excuse.
 
Wengine tumejikuta kwenye hilo jumba anasa tunaziona lakini hatuna uwezo wa kuzigusa, maana kuna "wababe" nao wamejikuta kama sisi humu lakini wamejiamulia kuwa ni vya kwao.

Tumeishia kuwa wapenzi watazamaji.

Mbaya zaidi tunaathiriwa na mtokeo ya maaumuzi ya wababe hawa hata ingawa hatuhusiki.

Tunaona mambo mengi ya kutisha na kuhuzunisha yanayofanywa na wababe hawa.

Tukawakimbia wababe tukiwa tumejaa majeraha na sonona tukajificha kwenye kabustani kako ndani ya eneo la kasri hili.

Huku tukijiuliza maswali mengi: tumefikaje hapa! Hivi vitu vya nani! Vya nini? Hapa kwa nani?

Ghafla tukaokota kakaratasi.

Mwenye jumba lake kaacha ujumbe mrefu sana!

Je unajua ni ujumbe alioacha mwenye jumba? ?

Hint: Kasema hizo anasa za humo si kitu kulinganisha na kile alichotutayarishia wakati akirudi.

Na wababe wakae mkao wa "kuliwa".

"Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona, wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao."
1Wakorintho.2.9.BHN
 

Acha bange Mkuu..

Aliomba wakati hakuwepo?
Unataka kusema alijiumba mwenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…