Sikupanga kuwa na mtoto...


Na sio wote wanaobeba mimba miezi yote tisa wanakuwa wamepanga mydia: Kuna wale wanaokuwa wanatamani kuitoa but may be wanagundua when it is too late kuitoa (Si nasikia kuna mwisho wa risks); kuna wanaojaribu na kukuta imegoma kutoka ........mtaani kuna usemi kuwa mimba ya mtoto wa kiume huwa ni ngumu sana kutoka; au wengine wanakwambia ukoo wetu hatutoagi mimba na ukiitoa ya kwetu lazimma ikuondoe na wewe au inagoma. Sasa huyu analazimika kuzaa kwa kuwa alijaribu kluitoa ikashindikana! au mie nachanganya madawa?
 

Kloro turudi kwenye “mtoto ambae hakupangwa“.....
 
Kloro turudi kwenye "mtoto ambae hakupangwa".....

To be honest hii term ya mtoto ambae hakupangwa ndo kwanza naiona leo..... ndio maana nikaona nielezee mimba ambayo haikupangwa.
Labda uifafanue zaidi ili tuende sambamba.
 
Lizzy na tama naomba niwakumbushe lile tendo si kwa ajili ya child production peke yake. Mtu anawezaenda for starehe kikanasa 'bahati mbaya kwa maana ya condom kutoboka, kusahau kumeza a pill, n.k

Na wengine ni kama stress releaser, starehe, e.t.c

MJ1 najua sana hilo mami...ndo maana hua nasema kama kweli mtu hataki kupata ujauzito either asifanye mapenzi ili kuepuka hata zile “bahati mbaya“ na kama akishindwa kabisa kujizuia basi akae akijua kwamba kuna uwezekano akaipata hata kama atakua mwangalifu.Hivyo kitendo cha kuamua kujihusisha kimwili na mtu mwingine tayari anakubali matokeo yake...yakiwa ni starehe..magonjwa pamoja na mimba.

Njia pekee ambayo inampa mtu uhakika wa kutopata mimba ni kutofanya mapenzi....hivyo watu waache kusingizia dawa ya penzi as if hawajui kwamba yaweza kupasuka...au siku zao as if hawajui mwili wake unajiendesha wenyewe na wakati mwingine mabadiliko hutokea!
 
<br />
<br /
Sasa unamshauri nini anayegundua ana mimba tayari wakati hakupanga?
 
Hapo red kama mtu yupo kwenye ndoa pia utampa ushauri huo?
 
Duh Lizzy hiyo Red utakuwa unatunyima haki zetu za kustarehe, have fun na tuwapendao ati!! Yaani kwa kuwa sitaki kupata mimba basi nisi'stareh"??!! ingekuwa hivyo si tungekuwa tunakutana wakati wa kutaka kureproduce tu?!!
 
lizzy, naomba unihabarishe kati ya mimba na mtoto kipi hutangulia? katika jibu utakalotoa, imani yangu mimi ni kwamba kile kitakachokuwa cha kwanza ndicho huamua mpango wa kile cha pili, Ila kumbuka pia kupanga ni kuchagua eeeh. Lakini pia watu wanapoamua kuzaa si kwamba wamepanga kwa kuridhika kabisa na hali hiyo , bali wanahofu juu ya maamuzi ya kutoa mimba ambayo huambatana na madhara anuai.
 
Hahahah...wala hujachanganya ...
I guess hapo mtu anakua hajajiandaa wala hataki kuzaa ila bado nashindwa kusema kwamba mtoto wake anakua hakupangwa...though inawezekana kwamba hivyo ndivyo.
 
Shemeji uko kwenye ndoa?!! Subiri mpaka mtake watoto hahahha......kama mnyama anavyosubiria mwenzake awe kwenye heat!!!
Shem kama hali yenyewe ndo hii! naona heri Lizzy anilejeshee mahari yangu. yaani kiduku sipati mpaka Lizzy atake mtoto. khaaa!
 
Sasa unamshauri nini anayegundua ana mimba tayari wakati hakupanga?

Ushauri wangu siku zote utaegemea kwenye kukubali majukumu....tatizo ni kwamba naweza kushauri ila nikawa napoteza muda tu!
 
Duh Lizzy hiyo Red utakuwa unatunyima haki zetu za kustarehe, have fun na tuwapendao ati!! Yaani kwa kuwa sitaki kupata mimba basi nisi'stareh&quot;??!! ingekuwa hivyo si tungekuwa tunakutana wakati wa kutaka kureproduce tu?!!

Hahahaha naona nimewagusa pabaya we na Kloro!!

Nwy nlichokua najaribu kusema ni kwamba ukiamua tu kufanya mapenzi jua kwamba uwezekano wa kupata mimba upo...na kama mimba kwako ni kitu ambacho kinaweza kukupa wakati mgumu sana basi amua kutoipa nafasi hiyo mimba itokee.

Kwahiyo furahini...furahishaneni ila ikitokea mimba msilie na kulalama as if ni muujiza.
 
Shem kama hali yenyewe ndo hii! naona heri Lizzy anilejeshee mahari yangu. yaani kiduku sipati mpaka Lizzy atake mtoto. khaaa!

Kloro mahari mbona imeshatumika...waweza kusamehe kama hutoweza kunivumilia.
 
Ukipenda Boga penda na uwa lake shemeji, ni sehemu ya mapenzi ati!!
hehehe mdosi yeye alisema "kipenda boga subiri mezi ya ramazani, waislam napenda sana"

On a serious note bado sijaelewa hii quote ya mtoto ambae hakupangwa, wallahi sitanii hii ni quote ngeni sana kwangu.
 
Mimba inatangulia.
Ofcourse kinachotangulia kwanza kinahusika kuamua kitakachotokea.Ila sio kila yai linakua kifaranga....na hapa ndo ujue kwamba choice ipo ya kuiruhusu mimba iwe mtoto au la.

Wanaacha kwa woga japo hawataki wanatakiwa wawe wanafikiria hayo yote kabla ya kujiachia na sio baada!
 
On a serious note bado sijaelewa hii quote ya mtoto ambae hakupangwa, wallahi sitanii hii ni quote ngeni sana kwangu.

Kloro bana....
Yani kabisa hujawahi kusikia mtu akisema “ahh sikupanga kua na mtoto mie...ilikua bahati mbaya tu“ ...?!Wapo sana na wengine hua hata wanasema mbele ya hao watoto!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…