Sikutaki tena - Dataz & Soggy Doggy

Sikutaki tena - Dataz & Soggy Doggy

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
DATAZ FT SOGGY DOGGY.
- SIKUTAKI

Intro..

( Soggy doggy)...

"Sikiliza dataz mi nimekuja tuyaongee tuyamalize nini lakini"

( Dataz..)

"Soggy umefuata nini kwetu nilishasema sitaki..

( Soggy doggy)

"Sikiliza dataz lakini mbona hivyo lakini Eeeh!!

( Datazi)

Nilikupa nafasi ukaichezea wakati ni ukuta umesha luka wako ovyo sitaki!!

( Soggy doggy)

"Dataz lakini samahani naomba unisamehe Datazi

(Dataz)

"Umenidanyanya mara ngapi? Nimekusamehe sikutaki Tena....

Verse 1. (Dataz)

"Ulikuwa usiku wa mkesha wa mwaka mpya/ ndipo nilipomfumania mpenzi wangu na kimwana kipya/ nikamuuliza samahani honey huyo ndio nani.. Ni nani...?/

( Soggy doggy)

"Usijali mpenzi mrembo wangu..!! Karudi juzi tu kutoka ujerumani...

(Datazi)..

"Kwa jinsi nilivyompenda na majibu aliyonipa/ aliniridhisha baada ya siku mbili, Tatu/ nikasafiri kuelekea Arusha/ rahasha!!.. mambo niliyoyasikia nikiwa huko/ yanasikitisha nikiwepo unasema unanipenda/ nisipokuwepo anani nyenyusha mashangingi wa kweli mpenzi/ wanakutia kiwewe kila kona wanakuta buzi/ toka masaki mpaka kawe/ mpenzi kumbuka ni wapi tulipotoka mimi na wewe/ sasa nasema hivi! Usinijue nakulia jiwe na lolote liwe/ heri niwe pekee yangu/ kwako sina Tena changu/ mimi sio size yako Tena/ ka angaike na machangu/ kijana unafanya mambo humuongopi hata mwenyezi Mungu/ unavunja amri ya sita, ya saba, ya nane, ya tisa na halafu Bado unataka uwe mpenzi wangu/ sikutaki Tena..!!

Chorus...

( Soggy doggy )

Baby I love 💕 u

( Dataz )

I hate u

( Soggy doggy)

I love 💕 u

( Dataz )

I hate u

( Soggy doggy)

I love 💕 u

( Dataz)

I hate u so much right now

( Soggy doggy)

Nakupenda

( Dataz)

Sikutaki ..!!

(Doggy doggy )

Nakupenda

( Dataz)

Sikutaki Tena.!!

( Soggy doggy)

Baby I love 💕

( Dataz )

I hate u

( Soggy doggy)

I love 💕 u

( Dataz)

I hate u so much right now

( Soggy doggy)

Nakupenda

( Dataz)

Sikutaki..!

( Soggy doggy)

Nakupenda

( Dataz)

Sikutaki Tena ..!!

Verse ..2 ( Dataz)

"Mapenzi yetu Enzi hizo yalikuwa kama ya kulwa na Dotto/ mimi nikiwa mkono wa
Kulia wewe unakuwa wangu wa kushoto/ mapenzi yetu Enzi hizo yalikuwa moto moto/ watu walikuwa wakitusifu jinsi tulivyokuwa na mapenzi ya mvuto/ tena mazito lakini nashangaa penzi letu limeisha kama lipasukavyo puto/ kumbuka mpenzi sikukupendea kidato wala kipato/ mara ya kwanza kukuona ulikuwa na baiskeli/ na leo hii una vito ulishangeuka soggy wa watoto/ I hate u, nakuchukia sitaki hata kukusikia/ mwanzo nilikuona nyama lakini leo hii kama ni mbonga wewe bamia/ hamu yote imeniishia timua ishia/ kacheze na viluka njia/ ulikuwa dreva ,utabaki kuwa abilia/ sikutaki Tena ..

( chorus) repeat .

Verse 3 ( Dataz)

Hakuna Tena kujuana/ kila ulichotaka nilisema Eeh bwana bwana!! / Ukaningeuza mpira ukanichezea ndanandana/ usikatee wewe ni muhuni kila mtu ana fahamu chukua time/ kula Kwa macho , kutesa kwa zamu/ waachie wenzio walio na hamu / ama kweli binadamu hapendeki/ mwenzio nakupenda unaningeuza tambala la deki/ sikutaki Tena../ labda kamfute Jackie huna kile unakitaka hata hiki/ uliponitaka ulisema nina kupenda sana / huna lolote kumbe unanindanganya bwana/ sikutaki Tena..

( Chorus..) Repeat..
🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶

End...

ukwaju_wa_ kitambo
0767 542 202
#funguk
1726457521179.jpg
 
Back
Top Bottom