Sikutegemea nilichokikuta ukweni

Ngengemkenilomolomo

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2015
Posts
270
Reaction score
450
Wakuu habari za muda huu.

Kijana wenu nina umri wa miaka 28. Baada ya kuona kwamba sasa yanifaa kuwa na mwenzangu wa kuishi nae basi nikachukua jukumu la kwenda kwao kujitambulisha na kufahamika rasmi ili basi niishi nae kihalali kabsa
Kipato changu sio kikubwa sana hvo nikawa nimejiwekea kias flan kama mahari (million 1) nikamwambia mwenzangu kwamba hima hima kaongee na mama kama ataweza kuongea na mzee bc mahari isizidi hapo.

Mwenzang akanifata na kunijulisha kwamba mzee amekubal lkn anaomba angalau basi iwe 1.5 ili waweze kugawana nyumban na baadhi ya ndugu kwakuwa natambua kwamba mahari huwa haiishi (baada ya kuelezwa na wakubwa wangu) bc nilikubali kulipa hyo 1.5 lkn kwa malipo ya kidogo kidogom.

Jana kwa neema ya Mungu ndugu na familia yangu wakaongozana hadi kwao na mwenzang kwa ajili ya kutoa kishika uchumba na pia kulipa nusu ya mahali tuliyokubaliana. Baada ya kufika huko ndugu zangu hawakuamin walichokutana nacho huko ambacho ht mm mpk sasa siamin bado.

Mahari wamekuta ni million 4 na mahitaji kama koti la babu na vitu vingine jumla million 2 yan TOTAL ni million 6.

Kwa bahati mbaya sikuwepo ila laiti kama ningekuwepo bc ningewaomba ndugu zangu turudi nyumban
Nimesikitishwa sana na kilichotokea jana japo ndugu wamenishauri nisioneshe nia ya kukataa kuendelea na binti huyo lakini naona kabisa sitoweza najiona nikimuacha na kuendelea na maisha yangu
Ukweni wamenionesha rangi halisi kwamba kwao pesa ndio kipaumbele kikubwa kulko upendo.

Roho imeniuma sana nimejitoa vitu vingi sana ukweni kabla ya cku ya jana malipo yake ni mahari ya kukomoana kiasi hiki.

Wakuu naombeni faraja zenu na ushauri wenu nifanye nini katika swala hili.

Natanguliza shukran🙏
 
Uislamu raha sana kwenye jambo kuoa moja mahari ni ya mwanamke yeye ndio anataja anataka nini kama seti ya sahani sawa kama mkeka wa kuswalia sawa ... Jambo la kuzika na jambo la kuoa limefanywa rahisi na la haraka mno .
Pole mkuu lipa hiyo mahari mambo ya mila ya ajabu ajabu waachie wenyewe
 
Kuna siku tulikwenda kumuwakilisha dogo kwenye kutoa mahari, Kuna kiasi elekezi tulichoambiwa, kufika ukweni kabla ya kula tukaingia kufanya negotiations kwanza. Wakwe wakatuona labda tuna pesa Sana wakapandisha kila kitu zaidi ya Mara nne kupunguza wamegoma. Sisi tukasema hebu tutoke nje tukatete halafu tunarudi kutoa mrejesho. Ile kutoka nje tukampigia muoaji simu kwamba Mambo huku si Mambo. Dogo akasema, Wala msirudi kuaga ingieni kwenye gari rudini acha wale chakula Chao wenyewe na Mimi nambwaga binti Yao. Kwani tutakutana nao wapi sisi kila mtu anatokea mkoa wake. Ndio ikawa binti arudi sokoni Tena kutafuta mchumba mwingine.
 
Mimi nilishajiwekea sheria mahari mwisho 1M, ikizidi hapo napiga chini. Videmu vyenyewe hivi vya siku hizi unakilipia mahari 8M baadaye unakikuta na njemba kitandani mnaanza kukatana mapumbu na kuuana na mwanaume mwenzio.

Na tunakoendea nitapunguza. Mambo yakizidi kuwa meusi nahamia team kataa ndoa
 
Jindanganye hivyo labda waislam wa mtaani kwenu ndo mahali anataja demu
 
Hao ni masikini wa kipato wanataka Binti yao awatatulie shida zao waIizolimbikiza miaka mingi Cha kufanya Mpe Binti yao mimba Kisha mtelejeze
 
Hii imekaa ki Mafia zaidi
 
Safi sana.
 
Milioni moja yote unatoa mahari mkuu? Dah, kweli wajinga hawawezi kuisha duniani.

Mahari ni laki mbili na inalipwa kwa awamu nne. Mahari zaidi ya laki mbili hao ni matapeli wanataka kumaliza shida zao kupitia binti yao.

Mnapofunga ndoa lengo ni kutengeneza maisha ya familia yenu sasa iweje mmoja awe kupe mwingine maumivu?
 
Kijana, dunia ya "upendo" ilipitwa na wakati, kinachopendwa sasa ni pesa tu, ama unazo unatowa yameisha, ama huna unasepa. Nduki.
 
Acha ubishi mkuu waislamu hawana mambo mengi kwenye suala la mahari hilo lipo wazi sio mambo ya kusadikika.
Acha ubishi.
Kuna waislamu makabila tofauti. Mfano kwa waislamu wa Bukoba kinachoangaliwa Ni Mila za kihaya. Kwa waislamu wa kizaramo uislamu ndio unaangaliwa.
Inategemea binti Ni muislamu wa wapi.
Unategemea muislamu wa kikuria adai mahari ya laki tatu? Au muislamu wa kijaluo adai mahari ya elfu hamsini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…