Sikuwahi kujua kama kumbe Watanzania mna roho mbaya kiasi hiki

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Yaani mnajua kabisa kwamba GENTAMYCINE siku zote naishi huku Kisiwani Puerto Rico na tokea jana tumekumbwa na Kimbunga kimoja kibaya sana kiitwacho Maria ambacho kimeharibu karibia miundombinu yote hapa na hali ni mbaya mno lakini sijamsikia hata Mtanzania mmoja kunipa pole. Nimesikitika na kuumia sana tu.

Nyumba niliyokuwa naishi maji yamejaa karibia yanafunika na tokea usiku wa jana nipo katika ukumbi mkubwa ambapo tumehifadhiwa kwa muda ili kupisha ujio wa pili wa Kimbunga Maria na ubaya zaidi kinaambatana na upepo mkali pamoja na mvua kubwa sana.

Kweli nimeamini kuwa ukitaka kuwajua Marafiki wa kweli subiria wakati wa matatizo ndipo utawajua na Mimi nasema leo wazi wazi kwamba kumbe Members wote wa JF siyo Marafiki zangu wazuri na wa kweli kwani sijaona hata mmoja wenu akinikumbuka Mimi mwana Puerto Rico na kunipa pole kwa Kimbunga Maria kilichotuharibia vibaya sana hiki Kisiwa chetu.

Nisalimieni sana huko Nyumbani Tanzania.
 
Pambana na hali yako tu

Huku TZ vyuma vilivyokaza ni zaidi ya hicho kimbunga Maria
 
Pole sana Mkuu. Lakini ninakushauri usitegemee pole na msaada kutoka huku kwa kuwa hicho kimbunga hatukuleta sisi. Kwa sisi tunasema tunakazana kujenga miundo mbinu, hizo nyumba zenu mtajenga wenyewe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…