SILASI ISANGI; KIKULACHO KI NGUONI MWAKO

Joined
Feb 25, 2021
Posts
11
Reaction score
9
Silasi kinachokuponza sijui ni uoga au kutokujiamini?
Umepewa nguvu na katiba ya kuteua wajumbe wa kamati tendaji, umemteua Ikangaa na Bayi hali ukijua kabisa kikwazo cha maendeleo ya mchezo wa riadha kwa miaka kibao ni Filbert Bayi. Sijui kwanini unamuogopa. Sasa ngoja nikwambie, Bayi ameshaapa lazima uondoke na hautamaliza muda wako wa madaraka. Hakukubali toka umeingia anasema huna sifa za kuongoza hicho chama, lakini mbaya hawez kukusimamia na unatishia maslahi yake. Mbaya zaidi John Bayo amemlalamikia kua wewe na Katibu wako ndio mmesababisha Bayo atoke kwenye umakamu. Bayo alikua kibaraka wa Bayi na ilikua inampa nguvu kubwa sana Bayi kwenye RT sas ammemtoa. Wakati Bayo anaendeleza mapambano kule Arusha na kwa wajumbe ambao ana ushawishi nao, pia kuna mtu anaitwa Machibya, huyu ni tapeli hana kazi wala kipato na wewe umeonyesha kua tishio kwake. Unahoji hoji sana vyeti vyake. Machibya na aliekua mpinzani wako wakat wa uchaguzi walijisalimisha kwa Bayi na hata sasa ni vijana wake. Kumbuka Bayi hakukuunga mkono kwenye uchaguzi. Sasa hawa ndio askari wa mstari wa mbele wanaratibiwa na Bayo.
Wewe na katibu wako mmekaa kama maboya na nakuahidi jipangeni maana mnapigwa kutoka ndani. Katibu wako hajui kitu kuhusu mchezo wa riadha, wala siasa za huu mchezo yupo yupo tu hata hajielewi ananenepeana tu, nawewe huna ujasiri wa kufanya jambo lolote. Ondoa huyo katibu weka mtu ataekusaidia.
Kosa kubwa ulilofanya ni kumkatalia Bayi mashindano ya Taifa kufanyika Dar mkayapeleka Arusha, lakini pili mmeikataa bajeti yake alioleta alipwe milioni sita kama Director wa mashindano na mkamlipa laki nane kama wajumbe wengine wa kamati tendaji. Mashindano ya Taifa yakifanyika Dar Bayi ndio alikua anatoa malazi kwa wachezaji, chakula pale kwenye shule yake, usafiri wa kuwapeleka viwanjani, seminar kwa wamuzi na Director wa mashindano. alikua anaondoka na mpaka milioni kumi na zaid mashindano yakifanyika Dar, wewe unakuja kumtoa na laki nane? Bayi hatokaa akusamehe hilo kamwe. Na hii vita ya kamisheni inayomtanguliza Benja ambae ni Kijana wake aliemtoa Arusha kuja kukimbilia Pwani kinara wake ni yeye. Anataka kuongeza nguvu yaje kwenye kamati tendaji kwakua katibu wa Kamisheni Andrew hamheshimu Bayi ndio Bayi ameamua lazima Benja arudi kwenye kamati tendaji. na Huu ni mwanzo. kama ana nia njema nawewe kwanini hakushauri kwa kukupigia simu badala yake anakuchambua hadharani kwe magroup ya whatsApp?

Vita ndio kwanza imeanza, jiandae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…