Silinde: Kila mwanafunzi apande mti mmoja, zoezi liwe endelevu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wakuu wa mikoa na wilaya wametakiwa kusimamia kila mwanafunzi kupanda mti mmoja kila mwaka katika shule za msingi na sekondari ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri sekta ya elimu ikiwemo kusababisha udumavu kwa watoto shuleni.

Pia, maofisa elimu wa mikoa na halmashauri wametakiwa kufufua vilabu vya mazingira katika shule zote nchini ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutunza mazingira.

Maagizi hayo yametolewa leo Januari 25,2022 jijini Arusha na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, David Silinde akizungumza katika mkutano mkuu wa nane wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara (REDEOA).

Amesema Taifa linapoteza zaidi ya hekta laki nne za misitu kwa mwaka kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo matumizi ya kuni katika shule hivyo utaratibu huo wa kila mwanafunzi kupanda miti utasaidia taifa kuondokana na njaa na ukame.

"Jambo hili la ukataji wa misitu linachangania mabadiliko ya tabia nchi, miongoni mwa athari hizo ni majanga ya njaa na ukame unaosababisha udumavu kwa watoto shuleni," amesema Silinde.

"Kutokana na changamoto hizo naelekeza kwenda kuimarisha shughuli za utunzaji wa mazingira katika shule zote nchini kwa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapanda mti mmoja au zaidi kila mwaka na kuutunza, wakuu wa mikoa na wilaya wote nchini wasimamie hili la upandaji wa miti katika maeneo yao".

"Nasisitiza upandaji wa miti liwe jambo endelevu. Kwa maofisa elimu wote muende mkafufue vilabu vya mazingira katika shule zote nchini ambazo zinawajenga watoto kuwa na uwezo wa kupenda mazingira angali bado wadogo na wao kama kizazi kijacho watakuwa wahifadhi wazuri,"

Kuhusu changamoto ya magari kwa maafisa elimu mkoa, Naibu huyo amesema Serikali imeshaagiza na kulipia magari 184 ambayo yanatarajiwa kuwasili nchini kuanzia mwezi ujao, lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya sekta hiyo muhimu.

Katibu Mkuu wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe amewapongeza maafisa elimu hao kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya madarasa mapya zaidi ya 15,000 huku akiwataka kusimamia vema miradi mingine inayotekelezwa katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo, Germana Mng'ao amesema kupitia mkutano huo wa mwaka wajumbe hao watajadiliana namna ya kuboresha sekta ya elimu.

Ameiomba Serikali kama ambavyo imeboresha shule kongwe za sekondari, ifanye ukarabati kwa shule kongwe za msingi ambazo nyingi zimechakaa.

Mwananchi
 
Angesema miti 100 kwa kila mwanfunzi kwa mwaka sawa Sasa kamti ndio nini

Kuna watu wawili tu Brazil walipanda miti milioni mbili kwa miaka 8 na kusaidia na jeshi na watu wengine milioni nne mingine

Kama tusipopanda miti mingi maana yake wanyama na ndege wataisha au kuhama
 
Mnapoongelea miti kumbukeni pia kupanda miti ya matunda. Miembe, mifenesi, stafeli, mipera nk. Licha ya kuleta kivuli, kutunza ardhi pia hutoa matunda yanayowafaa binandamu, wanyama na ndege.
 
Pandeni miti ya Asili inayorandana na Jiografia ya eneo....Pia Mtaala wa Elimu ya Mazingira should be established kuanzia Elementary mpaka Ordinary level...

Earthmover UNDP Mazingira consultant

CONGO DRC
 
Mnapoongelea miti kumbukeni pia kupanda miti ya matunda. Miembe, mifenesi, stafeli, mipera nk. Licha ya kuleta kivuli, kutunza ardhi pia hutoa matunda yanayowafaa binandamu, wanyama na ndege.
Hili lingekuwa jambo zuri sana. Kuna maeneo kama Songea, wamepanda miembe barabarani. Nafikiri ni wakoloni.
 
Wakuu wa mikoa na wilaya wametakiwa kusimamia kila mwanafunzi kupanda mti mmoja kila mwaka katika shule za msingi na sekondari ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri sekta ya elimu ikiwemo kusababisha udumavu kwa watoto shuleni.

Pia, maofisa elimu wa mikoa na halmashauri wametakiwa kufufua vilabu vya mazingira katika shule zote nchini ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutunza mazingira.

Maagizi hayo yametolewa leo Januari 25,2022 jijini Arusha na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, David Silinde akizungumza katika mkutano mkuu wa nane wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara (REDEOA).
Hili agizo lilimshinda JK miaka ya mwanzo kabisa ya uongozi wake alisema kila RC ahakikishe miti inapandwa kandokando ya barabara zote ndani ya mkoa wote
 
Angesema miti 100 kwa kila mwanfunzi kwa mwaka sawa Sasa kamti ndio nini

Kuna watu wawili tu Brazil walipanda miti milioni mbili kwa miaka 8 na kusaidia na jeshi na watu wengine milioni nne mingine

Kama tusipopanda miti mingi maana yake wanyama na ndege wataisha hizo sehemu za ukamwe
Ukamwe ndio nini?
 
Wakuu wa mikoa na wilaya wametakiwa kusimamia kila mwanafunzi kupanda mti mmoja kila mwaka katika shule za msingi na sekondari ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoathiri sekta ya elimu ikiwemo kusababisha udumavu kwa watoto shuleni.

Pia, maofisa elimu wa mikoa na halmashauri wametakiwa kufufua vilabu vya mazingira katika shule zote nchini ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutunza mazingira.

Maagizi hayo yametolewa leo Januari 25,2022 jijini Arusha na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) anayeshughulikia Elimu, David Silinde akizungumza katika mkutano mkuu wa nane wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Halmashauri Tanzania Bara (REDEOA).

Amesema Taifa linapoteza zaidi ya hekta laki nne za misitu kwa mwaka kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo matumizi ya kuni katika shule hivyo utaratibu huo wa kila mwanafunzi kupanda miti utasaidia taifa kuondokana na njaa na ukame.

"Jambo hili la ukataji wa misitu linachangania mabadiliko ya tabia nchi, miongoni mwa athari hizo ni majanga ya njaa na ukame unaosababisha udumavu kwa watoto shuleni," amesema Silinde.

"Kutokana na changamoto hizo naelekeza kwenda kuimarisha shughuli za utunzaji wa mazingira katika shule zote nchini kwa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapanda mti mmoja au zaidi kila mwaka na kuutunza, wakuu wa mikoa na wilaya wote nchini wasimamie hili la upandaji wa miti katika maeneo yao".

"Nasisitiza upandaji wa miti liwe jambo endelevu. Kwa maofisa elimu wote muende mkafufue vilabu vya mazingira katika shule zote nchini ambazo zinawajenga watoto kuwa na uwezo wa kupenda mazingira angali bado wadogo na wao kama kizazi kijacho watakuwa wahifadhi wazuri,"

Kuhusu changamoto ya magari kwa maafisa elimu mkoa, Naibu huyo amesema Serikali imeshaagiza na kulipia magari 184 ambayo yanatarajiwa kuwasili nchini kuanzia mwezi ujao, lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya sekta hiyo muhimu.

Katibu Mkuu wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe amewapongeza maafisa elimu hao kwa kusimamia ujenzi wa miundombinu ya madarasa mapya zaidi ya 15,000 huku akiwataka kusimamia vema miradi mingine inayotekelezwa katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja huo, Germana Mng'ao amesema kupitia mkutano huo wa mwaka wajumbe hao watajadiliana namna ya kuboresha sekta ya elimu.

Ameiomba Serikali kama ambavyo imeboresha shule kongwe za sekondari, ifanye ukarabati kwa shule kongwe za msingi ambazo nyingi zimechakaa.

Mwananchi
Kazi si kupanda miti kazi ni kuitunza mpaka ifikie kujitegemea
Labda kuwe na visima vya umwagiliaji ila kwa maji ya bomba bill zitawashinda
 
Mnapoongelea miti kumbukeni pia kupanda miti ya matunda. Miembe, mifenesi, stafeli, mipera nk. Licha ya kuleta kivuli, kutunza ardhi pia hutoa matunda yanayowafaa binandamu, wanyama na ndege.

Wazo zuri sana
Nakumbuka zamani kila nyumba kulikuwa na mti wa matunda
 
Back
Top Bottom