Silinde na Lijualikali jifunzeni kwa Zitto

Silinde na Lijualikali jifunzeni kwa Zitto

JERRY

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
630
Reaction score
502
Zitto alikuwa ni one of the Big Guns za CHADEMA, yaani kwenye top 3 unamkuta Mbowe, Slaa na Zitto; kipindi hicho hawa wengine kama kina Lissu, Lema na wengineo hawajaibuka kiivo, Kiufupi alikuwa moja kati ya Pillars za chama alipofutiwa uanachama Zitto aliendelea kuwa muungwana sana kwa namna fulani na hakupiga makelele na kutoa kashfa kwa chama au viongozi wake wakuu ndio maana hata leo CHADEMA haioni shida kuona namna ya kushirikiana na Zitto kwenye chaguzi.

Hawa jamaa Silinde na wenzake kwanza sio pillars za chama ivyo hawana athari lakini tangu watoke CHADEMA wamekuwa hawatulii ni kutukana viongozi wao wa zamani na kashfa kibao hawajui wao ni vijana na kama watabaki kufanya siasa safari ingalipo ndefu; Wekeni akiba ya maneno jifunzeni kwa Zitto.

Pia soma > Silinde ajifunze ''busara'' za Lijualikali
 
Utoto na ujinga vinawasumbua...iko siku mbeleni wakipata utulivu wa akili watajutia wanachokifanya leo!.

Ni sawa na demu anaachana na mpnz wake leo halafu kesho anatoka hadharani anasema jamaa yake alikuwa ana kibamia wakati waliishi kwa furaha miaka kibao bila tatizo lolote.

Wenye akili tutajua tatizo liko wapi.

Hata mwanaume mwingine makini ataogopa kukuoa tena maana anajua akili yako ni ile ile.

So hata Silinde na Lijualikali mnadhani mnawafurahisha sana ccm ila tambueni kwamba watu wote makini walio humohumo ccm wanawadharau sana kwa mnachokifanya leo!.

hata shuleni wakati tunafundishwa namna ya kuomba kazi tulisisitizwa sana kuepuka kumsema vby muajiri wako wa zamani...hata kama alikuwa na mapungufu.
 
Hawa vijana hawajakwiva kisiasa hata chembe, hata huko walikohamia wanaweza wasiaminike wala kupewa nafasi kwa kuwa kuna Sikh wakitoka watafanya haya wafanyayo leo dhidi ya chama walichotoka.

Hii ni sawa na mtu aliyekuwa kwenye mahusiano na mtu na muda wote akiwa kwenye mahusiano asiwe amewahi kuujua udhaifu was partner wake isipokuwa baada ya kuachwa.

Siasa ni maisha na sera za chama ndo zinazoweza kuwa kigezo mojawapo cha kumvutia mwanachama kutoka A kwenda B.

CCM ni taasisi kubwa ambayo ina hazina kubwa tangu kuasisiwa kwake na pengine inawezekana vyama vingine hujifunza na kuiga baadhi ya mambo.

Tabia ni kama ngozi, leo ukitoka CDM na kwenda DP utawasema vibaya CDM, kinyume chake pia ni kweli.
 
Katika siasa za Tz naomba siku moja aje atokee mtu mwenye hekima kama za Zitto na ujasiri Kama wa Tundu Lissu, Hawa kwangu ndio watabaki kuwa wanasiasa wangu bora.
 
Hawa vijana hawajakwiva kisiasa hata chembe, hata huko walikohamia wanaweza wasiaminike wala kupewa nafasi kwa kuwa kuna Sikh wakitoka watafanya haya wafanyayo leo dhidi ya chama walichotoka.

Hii ni sawa na mtu aliyekuwa kwenye mahusiano na mtu na muda wote akiwa kwenye mahusiano asiwe amewahi kuujua udhaifu was partner wake isipokuwa baada ya kuachwa.

Siasa ni maisha na sera za chama ndo zinazoweza kuwa kigezo mojawapo cha kumvutia mwanachama kutoka A kwenda B.

CCM ni taasisi kubwa ambayo ina hazina kubwa tangu kuasisiwa kwake na pengine inawezekana vyama vingine hujifunza na kuiga baadhi ya mambo.

Tabia ni kama ngozi, leo ukitoka CDM na kwenda DP utawasema vibaya CDM, kinyume chake pia ni kweli.
Huko walikoenda bila hela ya maana hutoboi. Wabunge karibu wote ni wafanyabiashara.
Walikonyea kambi wanaangalia potential yako wanakupigania unatoboa
 
Hao vijana ni washamba na malimbukeni ila kuna aibu inawasubiri soon
 
Uwezo wao wa kuona ni hafifu. Kupata mpenzi mpya haimaniishi unatakiwa kumponda wa zamani. Ni ujinga. Unahisi huyo mpenzi wa sasa atajiona spesho sana kwamba hatapondwa pindi mtakapotofautiana!!
 
Zitto alikuwa ni one of the Big Guns za CHADEMA, yaani kwenye top 3 unamkuta Mbowe, Slaa na Zitto; kipindi hicho hawa wengine kama kina Lissu, Lema na wengineo hawajaibuka kiivo, Kiufupi alikuwa moja kati ya Pillars za chama alipofutiwa uanachama Zitto aliendelea kuwa muungwana sana kwa namna fulani na hakupiga makelele na kutoa Kashfa kwa chama au viongozi wake wakuu ndio maana hata leo CHADEMA haioni shida kuona namna ya kushirikiana na Zitto kwenye chaguzi.

Hawa jamaa Silinde na Wenzake kwanza sio pillars za chama ivyo hawana athari lakini tangu watoke CHADEMA wamekuwa hawatulii ni kutukana viongozi wao wa zamani na kashfa kibao hawajui wao ni vijana na kama watabaki kufanya siasa safari ingalipo ndefu; Wekeni akiba ya maneno jifunzeni kwa Zitto
Hao wako sokoni wanajiuza ... na wanajua taste ya mteja wao ... If you know what I mean.
 
Hawa utoto, njaa na ushamba vinawasumbua.
 
Nimeshangaa sana dogo anamsema mbowe kuwa kalewa kadondoka wakati mimi ninafaili zake chafu zikiwemo ZA kulewa na kuanza kununua WATOTO WA WAPIGA KURA WAKE PALE KIBEREGE HOTEL NA KUANZA KUWAFILA nyie mwacheni sauti zipo tunangoja majira ataelewa tu
 
Zitto alikuwa ni one of the Big Guns za CHADEMA, yaani kwenye top 3 unamkuta Mbowe, Slaa na Zitto; kipindi hicho hawa wengine kama kina Lissu, Lema na wengineo hawajaibuka kiivo, Kiufupi alikuwa moja kati ya Pillars za chama alipofutiwa uanachama Zitto aliendelea kuwa muungwana sana kwa namna fulani na hakupiga makelele na kutoa Kashfa kwa chama au viongozi wake wakuu ndio maana hata leo CHADEMA haioni shida kuona namna ya kushirikiana na Zitto kwenye chaguzi.

Hawa jamaa Silinde na Wenzake kwanza sio pillars za chama ivyo hawana athari lakini tangu watoke CHADEMA wamekuwa hawatulii ni kutukana viongozi wao wa zamani na kashfa kibao hawajui wao ni vijana na kama watabaki kufanya siasa safari ingalipo ndefu; Wekeni akiba ya maneno jifunzeni kwa Zitto

Mfa maji hakosi kutapatapa. Hawa wamepanik, wanajua hawakuwa IQ kubwa kiasi hicho bali CHADEMA walikuwa wakiwabeba kila waendako. Wanajua kuwa CCM haina muda wa kuwabeba, hivyo hata uenyekiti wa mtaa hawawezi kupata huko.

Hasira zake ni kuishia kuitukana CHADEMA, bila kujua kuwa kufanya hivyo ni kujiharibia kabisa. Watoto hawa wamekwisha kisiasa. Wamsikilize Mrema- TLP, huwa analia na kusema sasa hivi CCM wamenishughulikia na kuniua kabisa kisiasa. Nao wapo katika hatua hiyo.
 
Back
Top Bottom