Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,887
I HAVE A DREAM: "ONE DAY I WILL HAVE A BIG TECHNOLOGY COMPANY IN OUR COUNTRY AND THE WHOLE WORLD"
Watakutumia kama muwa na kukutupa kule usiwe na faida. Baada ya kupata wanachohitaji kwako watakutupa kuleeee. Usione wanakuchekea ni wanafiki hao lengo lao ni kupata wanachohitaji kutoka kwako. Wanakupa maisha ya muda mfupi siyo ya kudumu.
Basi simama kwa miguu yako unauwezo wa kufanya chochote kikubwa. Unanguvu zaidi yao na wanakuhiaji sana kwa sasa. Jitambue sasa na uanze kuzifanyia kazi ndoto zako. Tumia mda wako vizuri kupangilia mambo yako.
Halafu kumbuka kunawatu lazima uachane nao iliuweze kufanikiwa. Si kila mtu wa karibu na wewe anafaa kuwa na wewe. Vile vile kumbuka kunawatu lazima ukutane nao ili mambo yako yaweze kwenda.
Simama kwa miguu yako maana hao ulio nao ni mabepari, hawana huruma, wamepanga mipango yao. Sasa basi usibweteke na hivyo vitu vya mda wanavyokupa. Hawana huruma hao watakutupa kama takataka. Wamejaa udhalimu wa kila namna, wanajua mambo yao tu.
Bado unanguvu sasa jitahidi kufanya mambo yako na kupangilia vizuri mambo yako kabla ya taa kuanza kufifia. Mda huu ndio mwafaka wa kupangilia maisha yako vizuri.
Simama kwa miguu yako.