Simba achaneni na Pablo

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
8,542
Reaction score
18,340
Wakuu nimesikia tetesi kwamba Kocha wa 2020 - 2021 Pablo Flanko Martine yupo Tanzania. Pablo alikuwa akizira zira, alikuwa akigombana na akina Wawa, anapigapiga Machupa, hajawahi kuwa na ubingwa wowote. Na limpira lake la kukimbia kimbia.

Kuna tetesi kwamba huenda akamalizana na Uongozi wa Simba kurudi kibaruani kama Kocha Mkuu.

Kumrudisha Huyu mtu ni kwenda kujihakikishia kushika nafasi ya tatu.

1. Yanga
2. Azam
3. Simba

Tujiandae kisaikolojia.

Ushauri
Ningetamani sana Simba wamrudishe Didier Gomez Darosa. Huyu ni moja kati ya Makocha wangu bora kabisa kuwahi kuwaona Tanzania. Ila kiherehere cha kumtoa Simba kwa uzembe wa Wawa kwenye mchezo wa Jwaneng Galax.

Kulikuwa na tetesi kuwa Simba imemalizana na kocha wa Vipers ya Uganda, Mabingwa wa soka nchini Uganda Robertinho Oliviera.

Kocha huyo ambaye amekuwa na msimu bora na klabu hiyo ya nchini Uganda na inaelezwa amewavutia mabosi wa Klabu ya Simba miamba hiyo ya soka nchini Tanzania. Kocha wa Vipers ni mzuri, ikishindikana Gomez.

NB: Simba waache ushamba wa kubabili makocha.
 
Mimi na rafiki yangu Kalpana tuna imani kubwa na kocha wetu Juma Mgunda aka Guardiola Mnene.

Kupitia Juma Mgunda, tuna uhakika wa kufika nusu fainali kwenye Champions League! Lakini pia tunaweza kuurejesha ubingwa wa Ligi kuu msimu huu kutoka mikononi mwa watani wetu.
 
Kocha alikuwa Kishingo. Yule jamaa alikuwa vzr sana.

Da Rosa alikuwa mweupe Sana, wengi tulidhani alikuwa kocha mzuri kutokana na jinsi timu aloyoipokea toka kwa Sven ilivyokuwa inacheza pira BIRIAN, aisee msimu ulivyoanza, akaenda pre season na timu yake aliyoisajili, ilirudi inacheza pira takataka
 
Banned

Unaisoma hii comment ukiwa guest na huna jeuri yeyote ya kuijibu
Acha roho mbaya mtani. Kuna watu wanatukana watu humu, halafu hawapigwi ban, wala nini.

Halafu ni wakati sasa wa kuwashauri wenye hii jamii forums, kuruhusu mjumbe aliyepigwa ban kuingia kama mgeni! Badala ya kumfungia hata kusoma tu mada zilizomo humu.

Haya ni manyanyaso ya wazi kabisa!
 
Siyo kwamba Pablo anaenda Azam fc!!??
 
Na mbaya zaidi Kuna watu wakikuripoti upigww ban haichelewi,hata Kama hapakua na mantiki ya ban,Kuna mjumbe nilimuuliza wewe kutwa na mada za chama chako pendwa,Kuna mtu twita naye kutwa mada za chama hichohicho,wewe ndiye huyo,akaniripoti eti nimemtaja jina nipigwe ban,nikapigwa wiki mzee,forum ya watu hii!!
 
Hizi ban zao zimekaa kisiasa siasa sana.
 
Kaka unajua boli sana na una jicho la kiufundi.

Sven ndio mtu aliekuwa nyuma ya uchezaji ule wa Simba ( Biryani football).
 
Ukipigwa ban bado unayo access ya kusoma mijadala except kuwa mchangiaji
 
Ukipigwa ban bado unayo access ya kusoma mijadala except kuwa mchangiaji
Mimi mbona waliponipiga hiyo ban yao ya wiki, ilikuwa nikijaribu tu kufungua inaniletea maelezo ya kupigwa ban! Yaani nilikuwa sina access yoyote ile hata ya kusoma kilichomo humu!!

Au moderator aliyenipiga hiyo ban alikuwa ni shabiki wa simba?
 
Nakuunga mkono na mguu pia

Yule Kishingo ni kocha haswaaa.
 
Nakuunga mkono na mguu pia

Yule Kishingo ni kocha haswaaa.

Gomezi Alikuwa anauelewano mzuri na wachezaji.

Alikuwa akiheshimika na Uongozi na wachezaji.

Alikuwa na MATOKEO mazuri Uwanjani.
Alikuwa na soka safi.

HAKUWAHI kuruhisu magori zaidi ya mchezo mmoja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…