Simba alining'ang'ania koromeo siamini kama niko hai

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Date::9/16/2008
Simba alining'ang'ania koromeo siamini kama niko hai

Na Martha Ndeki
Mwananchi

HAMIS Mgagara (40) mkazi wa Chanika Zingiziwa, mkoa wa Dar es Salaam, bado hajaamini kilichotokea baada ya kuokoka kutoka katika mdomo wa simba jike ambaye tayari alikuwa amemkaba koo kwa kutumia makucha.

Kisa hicho cha kutisha kilitokea majuzi kijijini Zingiziwa, baada ya mkulima huyo kushitushwa na kelele za mbwa waliokuwa wakibweka karibuni na kichuguu katika eneo la shamba lake hapo kijiji majira ya asubuhi.

"Kama si wanangu, Saleh Hamis na Said Hamis na mpwa wangu Seifu Chamwande kuninasua mdomoni mwa simba ningekuwa nimebaki jina," alisimulia Mgagara kwa shida ambaye amelazwa Wadi ya Sewa Haji wodi 29, Hospitali ya Taifa Muhimbili,

"Niliposogea tu, simba huyo ambaye alioneka kama mwenye mimba alinirukia shingoni na kuniangusha chali, akazamisha kucha zake kwenye koromeo, nikapiga kelele kuomba msaada kwa majirani na familia yangu," anasimulia huku akiwa amefungwa bandeji kichwani na mikononi.

Anasema baada ya kelele za kuomba msaada, watoto wake wawili, Saleh na Said na baadaye mpwa wake Seifu walikuwa wa kwanza kujitokeza kutoa msaada na hapo ndipo mapambano na simba huyo mwenye hasira yakaanza.

"Mwanangu Saleh alipoona simba ameng'ang'ania koromeo langu alimkabakabali simba ili niweze kujinasua. Katika harakati hizo simba aliweza kuninyofoa kidole cha pili kutoka kidole gumba mkono wa kushoto na kuvunja mfupa wa kidole cha kati,"anasimulia huku uso wake ukionyesha maumivu makali.

Baada ya Saleh kumkaba kabali mpwa wake Seifu aliyekuwa na jembe alitumia mwanya huo kumlima simba kichwani hadi kuniachia na kumvamia Seif miguni kwa kulipiza kisasi kutokana na hasira ya kulimwa na jembe kichwani.

"Nami pia nilitumia mwanya huo kunyanyuka na kuendelea na mapambano na simba kwa kumpiga kwa jembe na panga hadi akaishiwa nguvu na kufikia hatua hiyo wanakijiji waliowahi kufika eneo la tukio waliendeleza mapambano hadi kummalizia, sisi tukiwa tayari tumechoka".

Baada ya mapambano hayo yasiyo ya kawaida, wanae walipata walipata matibabu na katika Hospitali ya Aman, Ilala, Jijini na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kuonekana kuwa hawakuwa na majereha mabaya kama aliyopata yeye, anasema.

Pamoja na majeraha ya koromea na mikono anasema anajisikia maumivu makali ya kucha za simba katika eneo la mashavu hali inayomfanya kuzungumza kwa.

Hata hivyo majeruhi huyo mwenye bahati ya kuokoka kifo anasema anawashukuru waganga pamoja na wahudumu wa Muhimbili kwani wamempokelea vizuri na kuwa amepatiwa matibabu yanayompa imani ya kupona haraka.

Afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jezza Waziri, anasema majeruhi walifikishwa hapo katika hali mbaya kwa kuvuja damu kwa wingi kutokana na majeraha makubwa lakini hali yake ilikuwa inaendelea vizuri tofauti na juzi.
 
Mie nilifikiri huyu ni Sophia Simba. Ehhh, kumbe ukisikia Simba kweli mpishie mbali. Naona hii ni wiki ya Simba. Poleni wanafailia na Hongera kwa ushujaa...
 
Shujaa sana huyo Mzee na watoto wake...wengine hapo mweeeeee wangesubiriaa msibaa tu mzee kaliwa Simba nje nyumba yake....huo ni ushujaa sana na inabidi tuwe ujasiri wa kukabilina na majanga mazito kama hayoo...sio nyumbani tu hata kwenye serikali yetu.....kama Baba mwenye nyumba hawezi kupambana ana kwa ana na adui...huyoo hawezi kuwa baba mwenye ujasiri ................kuongoza nyumba kwa ujasiri na uwezo wa kusifiwa na kuigwa...............JE Mwenyekaya wetu anaweza kupambana na Simba wa ufisadi?Inabidi tujifunze sio kwa kupiga makelele kuomba msaada kwanza tunajisaidia wenyewe kwa ujasiri na kupambana...baadae ndio unaomba msaada..hata kwenye kuongoza nchi tuige mfano huu wa ujasiri yasiishie kwa kusema du jamaa jasiri sana.....wewe kama mkuu wa kaya ujasiri wako nini??????
 
BaK ... this is a nightmare cant imagine .... God! sikuzake zilikuwa bado
 
Niliiruka hii post nikijua ni mambo ya Sophia Simba. Si utani, hii ni wiki ya Simba!



.
 
Mie nilifikiri huyu ni Sophia Simba. Ehhh, kumbe ukisikia Simba kweli mpishie mbali. Naona hii ni wiki ya Simba. Poleni wanafailia na Hongera kwa ushujaa...
Hata mie nilifikiria hivyo - kumbe!
Jamani majina mengine tuwe macho nayo! Jina hushabihiana na mwenye jina kwa kiasi kikubwa.Tizama majina - Sungura ( mjanja) Mbogo ( mkali) Sijali ( hajali kweli) Shida, Furaha, nk yanajieleza.
 
LOL! Mmenichekesha kweli 🙂. Lakini kama ulisikia bondia Sophia Simba alivyorumrushia makonde mgombea mwenzie wa kiti cha UWT halafu ukiona hiki kichwa cha habari basi unaweza kudhani kinahusiana na bondia Sophia Simba. Angekuwa anawapiga makonde mafisadi wengi tungemuunga mkono 🙂
 
Du hii inatisha pole zake huyo mzee!kweli ameokoka kwenye mdomo na makucha ya simba!MUNGU ampe afya njema!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…