pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,913
- 13,876
Habari zenu wadau wa soka na mashabiki kwa ujumla hongera kwa yanga sport club kwa kushinda mechi yao ya mwisho na kukaa kileleni kwenye msimamo wa NBC premier league.
Wakuu leo tuongelee mabadiliko ya kiuchezaji ya Simba sports club toka iwe chini ya kocha mgunda imebadilika sana ikiwa na mpira na hata ikiwa haina mpira.
Simba ya zamani ilikuwa ni ngumu sana kuona mchezaji kama chama anacheza aina ile ya mpira chama amebadilika siku hizi ana kaba anapopoteza mpira tofauti na chama yule tunayemjua anayesubiria wenzako wakabe wampe mpira sasa hivi ni kawaida kwa chama kumalizika mechi na kadi ya njano na anarudi mpaka nyuma kusaidia team isipokuwa na mpira.
Pape sakho pia amebadilika sana kwenye mechi ya jana sakho alipata kadi ya njano baada ya kuokoa mpira dhidi ya mpinzani aliyekuwa anaelekea langoni kwa simba upande ule wa shomari kapombe na yeye imekuwa kawaida kumaliza mechi na kadi ya njano.
Simba inacheza ki team wanarudi wote wakiwa hawana mpira na wanakuwa hatari kwenye counterattack toka iwe chini ya juma mgunda ukiangalia kuanzia ile mechi ya kimataifa dhidi ya de agosto unaona utofauti simba ya mgunda inahitaji pasi mbili au tatu mpaka tano kufika kwa mpinzani lile pira biriani la simba walilokuwa wanapiga lakini wanasumbuka kupata matokeo baadhi ya mechi limepotea,
sasa hivi pasi tatu tu simba ipo kwenye eneo la mwisho la mpinzani kuanzia goli lilofungwa kwenye mechi ya kimataifa dhidi ya de agosto mechi ya premier league dhidi ya yanga ukiangalia na mechi ya jana ile pasi ya mkude na mzamiru yasin hakuna goli lililofungwa ambalo shambulizi lake linalozidi pasi zaidi ya tano simba imekuwa hatari kwenye counterattack chini ya juma mgunda.
Wana simba tumpe support juma mgunda kwa aina yake ya uchezaji wa simba akiongezewa wachezaji wengine kumpa support anaweza kutufikisha mbali kwenye league ya ndani na kwenye champions league.
Simba imekuwa na balance inapokuwa na mpira na isipokuwa na mpira kipindi cha nyuma team ilikuwa dhaifu isipokuwa na mpira ila kwasasa kila mchezaji ana jukumu la kukaba team inapokuwa haina mpira sio moses phiri sio chama wala sakho kila mtu anatafuta mpira wana simba na watanzania tumpe support juma mgunda hata team inapopata matokeo mabaya kwani hakuna team duniani ambayo haifungwi,
ila uzuri wa mgunda ni msikivu sana kwa mashabiki na kwa viongozi wake akiendelea hivi atafika mbali na simba nipo na mgunda afungwe au ashinde nipo pamoja naye namatakia kila la kheri pep Guardiola mnene anaendelea kutengeneza CV na records akiwa simba sports club hata akiondoka simba leo hawezi kukosa team Tanzania na Africa kwa ujumla CV yake sasa hivi ni kubwa sana ukilinganisha na wenzake wengine wazawa na sisi tunasema SIMBA NGUVU MOJA.
NB:Mgunda ndiye aina ya kocha simba iliyokuwa inamuhitaji kwanza msikivu na anampa nafasi kila mchezaji kuonyesha uwezo wake asipopangiwa kazi na mamluki kina matola simba itafika mbali chini ya uongozi wake.