Simba, Chui, fisi ‘waingia’ Zanzibar

Simba, Chui, fisi ‘waingia’ Zanzibar

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Unguja. Wakati wanyamapori hususani simba na chui wakivushwa kwa mara ya kwanza kwenda kisiwani Zanzibar katika maonyesho ya tamasha la Kizimkazi, Ofisa Utalii kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), Lusajo Nsweve, akisemani mpango katika kutanga utalii.

Wanyama hao ambao kwa mujibu wa Nsweve ni mara ya kwanza kupelekwa kisiwani humu tangu uhuru, wananchi wamevutiwa kuwaona huku wakiomba kuwapo eneo maalumu la kudumu la wanyama hao na kivyo kutoa fursa kwa wengi kuwaona.

Nsweve ameyasema hayo leo Agosti 25, 2023 eneo la Paje Mkoa wa Kusini Unguja ambapo linafanyika tamasha la Kizimkazi, linalotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kulifunga Agosti 31, 2023.

Tamasha hilo lilianzishwa rasmi mwaka 2016 likitambulika kwa jina la Samia day kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2018 na kuitwa ‘Kizimkazi Day’ lengo likiwa ni kutangaza utamaduni, vivutio na rasilimali za Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja ambapo hufanyika kila mwaka mwezi Agosti.

Ofisa huyo wa Tawa amesema kuwa katika kuunga jitihada za Serikali kutangaza utalii Tawa imeamua kupeleka wanayama hao ikiwa ni kivutio kimojawapo kwa wanananchi hao sambamba na kuwapa burudani.
“Tunaendelea kutangaza utalii kwa nguvu zote lengo kubwa kuongeza idadi ya watalii na mapato kama ambavyo inajulikana kwamba sekta inayochangia pato la taifa zaidi ya silimia 17 ni utalii na inaongeza ajira rasmi na zisizo rasmi zaidi ya ajira milioni 1.5,” alisema.

Amesema hiyo ni fursa kwa wananchi kwa sababu inaweza kutoa pato binafsi na pato la taifa na kwamba ndiyo maa Tawa wamekuja kutoa elimu ya jinsi ya kuwafuga wanyamapori hao kupitia mashamba ya wanyama hao (zoo).

Wanyama waliovushwa kuja Zanzibar ni pamoja na simba, chui, fisi, pundamilia, pofu, nungunungu na ndege aina ya korongo.

“Ukiachilia mbali kuwaona kwenye picha, sijawahi kuwaona wanyama hawa kwakweli, nimevutika kuona kwa macho yangu, nimefurahi kweli,” amesema Khamis Rashidi mkazi wa Paje Zanzibar.

Kwa upande wake Khadija Fahma, pamoja na kueleza furaha yake ya kuwaona wanyama hao kwa mara ya kwanza, ameishauri Serikali kungalia uwezekano kuweka hifadhi kisiwani humo ili iwe rahisi na kutoa fursa kwa wananchi wengi kuwaona wanyama hao fahari ya Tanzania.

Kura zarudiwa tena uchaguzi KKKT
 
Kumbe kila rais anatamani jimboni kwake kuwe na mbuga za wanyama?, basi hakuna haja ya kumlaumu yule wa chato.

Mwisho wa siku Tanzania nzima itazungukwa na wanyama pori kila mahali! Wenye mahotel waweke vivutio, wenye nyumba zao zenye nafasi nao wapewe vibali waweke simba, nyati, swala nk kuvutia wageni wao.
Nchi ni yetu sote
 
Awamu hii ya wamakunduchi kila kitu cha Tanganyika kinapelekwa kwao kwa gharama za watanganyika.cha Tanganyika ni cha wote lakini cha kwao ni cha kwao.Hovyo sana nchi hii

Maisha yenyewe ni mafupi, utakufa utaacha kila kitu, so acha kulalamika. Muhimu kama wamepelekwa kwa njia ya halali sioni kama kuna shida.

Kuna watanzania wanakera sana, kila kitu wanataka wao tu wamiliki, wengine sio binadamu!
 
Kwa kuwa maisha mafupi ndiyo iwe cha zanzibar ni zanzibar na Tanganyika ni cha wote?
 
Mkapa Kuna mitambo ya kufua umeme ya mjerumani aliichukua msoma sijui aliipeleka mtwara. Wanaojua hii kitu kiundani please share something
 
Hahaah mkuu umewaza nini? Chui mshenzi sana anapiga miguu yote na mikono yote aisee
Kana viwembe 20 kwenye miguu yake.. Ongezea na meno.. Hakana adabu kabisa hako kajamaa.. Kana uwezo wa kufinya watu hata mia na msikapate na marungu na mawe yenu.. Nimewaza tu endapo katatoroka kutakuwa na msalie mtume hapo..??
 
Unguja. Wakati wanyamapori hususani simba na chui wakivushwa kwa mara ya kwanza kwenda kisiwani Zanzibar katika maonyesho ya tamasha la Kizimkazi, Ofisa Utalii kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), Lusajo Nsweve, akisemani mpango katika kutanga utalii.

Wanyama hao ambao kwa mujibu wa Nsweve ni mara ya kwanza kupelekwa kisiwani humu tangu uhuru, wananchi wamevutiwa kuwaona huku wakiomba kuwapo eneo maalumu la kudumu la wanyama hao na kivyo kutoa fursa kwa wengi kuwaona.

Nsweve ameyasema hayo leo Agosti 25, 2023 eneo la Paje Mkoa wa Kusini Unguja ambapo linafanyika tamasha la Kizimkazi, linalotarajiwa kufunguliwa kesho na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kulifunga Agosti 31, 2023.

Tamasha hilo lilianzishwa rasmi mwaka 2016 likitambulika kwa jina la Samia day kabla ya kubadilishwa jina mwaka 2018 na kuitwa ‘Kizimkazi Day’ lengo likiwa ni kutangaza utamaduni, vivutio na rasilimali za Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja ambapo hufanyika kila mwaka mwezi Agosti.

Ofisa huyo wa Tawa amesema kuwa katika kuunga jitihada za Serikali kutangaza utalii Tawa imeamua kupeleka wanayama hao ikiwa ni kivutio kimojawapo kwa wanananchi hao sambamba na kuwapa burudani.
“Tunaendelea kutangaza utalii kwa nguvu zote lengo kubwa kuongeza idadi ya watalii na mapato kama ambavyo inajulikana kwamba sekta inayochangia pato la taifa zaidi ya silimia 17 ni utalii na inaongeza ajira rasmi na zisizo rasmi zaidi ya ajira milioni 1.5,” alisema.

Amesema hiyo ni fursa kwa wananchi kwa sababu inaweza kutoa pato binafsi na pato la taifa na kwamba ndiyo maa Tawa wamekuja kutoa elimu ya jinsi ya kuwafuga wanyamapori hao kupitia mashamba ya wanyama hao (zoo).

Wanyama waliovushwa kuja Zanzibar ni pamoja na simba, chui, fisi, pundamilia, pofu, nungunungu na ndege aina ya korongo.

“Ukiachilia mbali kuwaona kwenye picha, sijawahi kuwaona wanyama hawa kwakweli, nimevutika kuona kwa macho yangu, nimefurahi kweli,” amesema Khamis Rashidi mkazi wa Paje Zanzibar.

Kwa upande wake Khadija Fahma, pamoja na kueleza furaha yake ya kuwaona wanyama hao kwa mara ya kwanza, ameishauri Serikali kungalia uwezekano kuweka hifadhi kisiwani humo ili iwe rahisi na kutoa fursa kwa wananchi wengi kuwaona wanyama hao fahari ya Tanzania.

Kura zarudiwa tena uchaguzi KKKT
Imeisha Iyo 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom