Simba Sports Club a.k.a wahenga inashuka leo kukabiliana na kikosi Azam kwenye uwanja wa Azam huko Chamazi. Simba inashuka kwa mara ya kwanza kwenye uwanja huu kuikabili Azam huku kila timu ikiwa na ubora na nguvu ktk maeneo tofauti tofauti.
Simba, ni dhahiri ndio wanaopewa nafasi kubwa kujizolea pointi 3 muhimu kutokana na kuwa na kikosi bora zaidi kwa sasa kuliko timu yoyote nchini. Imesheheni kila eneo na ina mseto mzuri wa ubora, vipaji, uzoefu na ufundi ndani na nje ya uwanja. Imejipanga na tayari imeonyesha dhahiri kuwa inataka kutawala soka la nchi hii.
Wakati Simba ikipewa sifa hizi na ikijiamini kupita kiasi, kuna kosa kubwa ambalo wao pamoja na wadau wa mpira wanalifanya, ambalo ni kutokuielewa au kutoifuatilia vizuri Azam FC, na hivyo kutopewa sifa inazostahili kwa maana ya ubora hasa baada ya kuondokewa na rundo la wachezaji wake waandamizi waliojiunga na Simba pamoja na Yanga. Nimeifuatilia Azam wakati wa maandalizi na naweza kukiri ndio timu iliyofanya maandalizi bora zaidi nchini.
Kwa yule aliyefuatilia pre-season ya Azam, atakubaliana kuwa wamekuja kivingine na ni sahihi kusema wameongezeka ubora zaidi kuliko msimu uliopita. Na hii ni ajabu sana kwa sababu tulitazamia baada ya kuondokewa na wachezaji nguli azam ingekuwa dhaifu kabisa msimu huu! Azam ya sasa ina kasi, inacheza kwa nguvu, malengo na wachezaji wake wanajitoa kwa 100% na ni vijana huku wazoefu wachache wakiowanyesha njia vijana. Vijana hawa wa Azam wananjaa mno na mpira.
Nimeshuhudia Azam ikizitoa kamasi timu karibu zote bora za Uganda ilizocheza nazo ikiwemo timu ya Taifa!! Walikuwa wakicheza vizuri mno na kwa mbinu bora kabisa za kujilinda, na kushambulia kwa kushtukiza na kasi kubwa. Waganda ambao mara nyingi huziwezea timu za bongo hasa ktk matumizi ya stamina, nguvu na ubabe, walijikuta wakidhalilishwa sana na vijana hawa waliokuwa wanafunga magoli mengi ya 'kideo' hususani mashuti ya mwendokasi. Yahaya Mohamed ndio alikuwa akiongoza mauaji ya kimya kimya na alikuwa akifunga kutokea upande wowote wa uwanja bila kujali amekabwa au la!
Azam iko vizuri kwenye kujibu mashambulizi na hapa walinzi wa Simba watapaswa kuwa ktk ubora wao wote kwa kuwa ni dhahiri Simba itatawala mpira lakini Azam inaweza kufunga mapema zaidi kuliko Simba na hata kuongeza mabao na kuwaacha wanamsimbazi na mshangao mkubwa.
Azam ni washindani halisi msimu huu. All in all kama timu zote zitacheza kwa ubora wao wote tunatazamia kuwa na mechi bora zaidi msimu huu.