Simba dhidi ya Ruvu Shooting: Clotous Chota Chama onyesha uungwana

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Kesho katika Mechi ya Simba dhidi ya Ruvu ataonekana mwamba Clotius Chota Chama (Triple C) ambaye hajaonekana uwanjani si kwa sababu ya majeraha au kiwango kushuka, ila ni kwa sababu hakusalimia wachezaji wa timu pinzani.

Sijui kanuni za TFF ila najiuliza kama Chama angekataa kumsalimia Muzamiru angepewa adhabu gani? Lakini haha hivyo tuliache hilo.

Kesho ili kuonyesha kwamba wewe mwamba wa Lusaka ni muungwana, kabla ya Mechi panda jukwaani ukawasalimie viongozi wote wa TFF watakaokuwepo, ukimaliza shuka lamsalimie Mkwasa na benchi lote la Ruvu, kisha nenda upande wa mashabiki wao wapungie mkono.

Na kwa vile Ruvu Shooting inatokea mkoa wa Pwani, ukionana na mtu yeyote anayetoka Kibaha mpe shikamoo yake, yasije yakakukuta tena yaliyokukosesha nafasi ya kutumikia timu yako.
 
hivi najiuliza kama tukio hili angefanya chama peke yake bila ya aziz ki kufanya wangemfungia chama, au angefanya aziz ki peke yake na chama asingefanya wangemfungia aziz ki pekae yake. au kitendo hicho angefanya kibu denis na azizi ki wangewafungia wote? TFF ni wajinga sana, wanapenda kubalance mambo. ndio maana simba walijitoa sportpesa na kwenda M bet kwa upuuzi kama huu.
 
Tunapeleka soka kwenye mambo ya kijinga halafu wakati huo huo tunataka kufanikiwa kwenye mpira.!

Unawezaje kumfungia mchezaji game Tatu kwa kosa la Fair Play kama vile amefanya Kosa la kuhatarisha afya ya mchezaji mwenzake ilhali ni Far Play. Wapi Fair Play ikawa lazima..!
 
Na asalimie uwanja mzima na mashabiki wote
 
Kuna siku mchezaji atafungiwa mechi 3 kwa kumrushia mpira mchezaji wa timu yake mpira uliotolewa na mchezaji wa timu pinzani kupisha kuhudumiwa mchezaji alieumia kiwanjani.
 
HII LIALIA HAITAWASAIDIA KITU,BOLI LITEMBEE LA SIVYO MTASHIKA NAFASI YA 4 MSIMU HUU OHOOO
Ule ngada alafu ushike nafasi ya nne?

Hawa watakua chini huko wanapambana wasishuke daraja!
 
Balancefication! Hata mimi naiona sana katika maamuzi ya TFF. Abadan angekuwa wa upende mmoja hii isingetokea. Mpira hauendi hivyo
 
Maoni yako yako sawa 100%
 
Kuna siku mchezaji atafungiwa mechi 3 kwa kumrushia mpira mchezaji wa timu yake mpira uliotolewa na mchezaji wa timu pinzani kupisha kuhudumiwa mchezaji alieumia kiwanjani.
Kwa TFF hii ya wahuni sitashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…