Simba hiki ni kipindi cha usajili. Je, mnasajili kwa kutumia ripoti ya Mgunda ama mnasubili kocha mpya?

Simba hiki ni kipindi cha usajili. Je, mnasajili kwa kutumia ripoti ya Mgunda ama mnasubili kocha mpya?

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Moja ya vitu ambavyo Simba na viongozi wake wanaferi ni eneo la usajili, sasa hivi wanaongelea kusajili lakini wakati huo huo hawana majibu kama mgunda wanampa timu ama lah!

Kama Mgunda anapewa timu basi wafanye usajili kupitia ripoti ya Mgunda, na kama wanatafuta kocha mpya wanatakiwa wampate kocha kwanza ndio atoe mapendekezo yake kulingana na mfumo wake anaopenda kutumia na aina ya wachezaji anaowataka kuwatumia ili wafit kwenye mfumo wake!

Huwezi kutumia ripoti ya kocha mwingine kumsajilia wachezaji kocha mwingine maana ujui huyo kocha mpya atahitaji wachezaji wa aina gani ili wafiti kwenye mifumo yake!

Kwa maana hiyo Simba kama anataka kufanya mambo kiuweledi anatakiwa apate kocha mpya kwanza na yeye ndio atoe mapendekezo ya usajili, vinginevyo yatakuwa yanajirudia yale yale ya kocha kuwapiga benchi wachezaji waliosajiliwa kwa gharama kubwa kwa kuwa atawaambia hawafit kwenye mifumo yake!

Kama Mgunda anapewa timu haina shida ripoti yake itumike lakini kama anaondoshwa iyo report haina maana!

Ni ushauri tu tunawapa mkipenda mchukue mkipenda mnaacha!
 
Haya mambo yaachwe kama yalivyo, kwasababu sio Simba pekee bali hata Yanga wenyewe haijajulikana hatma ya Gamondi. Gamondi ameshamaliza mkataba wake na Yanga na anaenda zake mapumziko. Sasa haijulikani kama atarudi kuendelea na Yanga au ndio watashindwana lakini Yanga inaendelea kusajili hata kama bado hawajajua hatma ya kocha ipoje. Kitu kinachoibeba Yanga kwasasa ni kujua falsafa yao ya mpira hivyo hata akiondoka kocha wanajua wazi kabisa kocha anayekuja atakuwa ni muumini wa soka la namna gani.
 
Wote pale Simba ni makanjanja watupu!
Hiki ni kipindi chao cha kufanya DHULUMA!
Wanamleta Mchezaji na tunadanganywa gharama yake kumsajili ni 700M kisha yeye anapewa 150M nyingine wanakula makanjanja!
 
Haya mambo yaachwe kama yalivyo, kwasababu sio Simba pekee bali hata Yanga wenyewe haijajulikana hatma ya Gamondi. Gamondi ameshamaliza mkataba wake na Yanga na anaenda zake mapumziko. Sasa haijulikani kama atarudi kuendelea na Yanga au ndio watashindwana lakini Yanga inaendelea kusajili hata kama bado hawajajua hatma ya kocha ipoje. Kitu kinachoibeba Yanga kwasasa ni kujua falsafa yao ya mpira hivyo hata akiondoka kocha wanajua wazi kabisa kocha anayekuja atakuwa ni muumini wa soka la namna gani.
Yanga ni tofauti sana na timu nyingine kwa sasa, uyo gamond ata Kama akiondoka yanga atatafuta kocha mwingine ndiye atakuja kusajili kwa kuwa ni kipindi Cha mapumziko ligi imesimama, lakini Simba ni tofauti mpaka Sasa awajui wampe mgunda ama watafute mwingine na wakati huo huo Wana lundo la wachezaji wanataka waache na wasajili lundo lingine
 
Baada ya Nabi kuondoka, kipi kilianza kwa Yanga kati ya ujio wa Gamondi au usajili wa Yao, Pacome, Max, n.k? Tusidanganyane timu zetu za Tanzania haziwezi kusajili kwa matakwa ya kocha kwasababu mfuko haupo vizuri. Kinachofanyika kocha anasajiliwa wachezaji anawakuta. Kilichopo hapa ni timu ipi inayofanya scout vyema ila hakuna timu ya Tanzania inayomwachia kocha ndio asajili
 
Kocha aliyemaliza msimu na timu ndio anayetoa ripoti kwa kamati ya usajili
Simba ina scout na ina kamati ya usajili hivyo kazi ya kocha ni kuainisha tu aina (sio majina) ya wachezaji anaowahitaji kwenye nafasi fulani zenye mapungufu then kamati wakiongozwa na scout watafanya usajili
 
Asikudanganye mtu, Tanzania hatusajili kwa matakwa ya Kocha bali, utashi, matakwa na uwezo wa kiuchumi wa timu kwa mujibu wa viongozi!
 
Back
Top Bottom