Simba ianze kutumia zaidi jezi nyeupe maana bado hazijachafuliwa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kuna kitu nimekiona msimu huu katika performance ya mchezaji mmoja mmoja wa Simba kimenifikirisha sana.

Katika michezo miwili ya msimu huu ambayo naikumbuka mpaka sasa Simba wakivaa jezi nyeupe, huu mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union na ule wa Costantine kule Algeria, performance ya mchezaji mmoja mmoja ilikuwa nzuri sana. Touch za wachezaji zilikuwa nzuri na mimi ndiyo kitu cha kwanza nakiangalia nikifanya tathmini ya performance ya mchezaji.

Inawezekana kabisa rangi nyekundu ya Simba imefanyiwa yale mambo ya kiutamaduni na inabidi kwanza isafishwe. Ukitaka kujua rangi nyeupe bado ni "takatifu" angalia jinsi upande wa pili wanavyoikumbatia.

Kuna mtu siku moja aliwahi kuliongelea hili suala, nimejaribu kutafuta ule uzi wake sijaupata.

Wasiwasi ni akili.
 
Ndugu mpira ni uwekezaji mambo ya rangi ni unajimu.

Wewe uwe na Aziz k, Pacome, Max, Mzize, Aucho, Chama, Job n. K wawe na utimama mzuri wa akili na Mwili, Bench la Ufundi liloshiba kweli uta anza kuchagua rangi za kuvaa!!!

Ata mkicheza tumbo wazi mtashinda tu, ikitokea kupoteza ni marachache sana.
Tujikite kwenye uwekezaji mambo ya kisayansi hayataki ubashiri.
 
Hao wachezaji uliowataja hapo wanakuzwa Sana ila hakuna kitu. Wote walikuwemo uwanjani wakati Yanga wanashindwa kuifunga MC Alger hata goli moja tu kwa dakika zote 90 za mchezo.
 
Nimeona nisijisumbue kumjibu huyo na post zake ya kukariri. Wachezaji anaotamba nao walishindwa kuifunga MC Alger hata goli 1 kwa dakika 180.

Kukumbushia tu dakika 180 ni masaa matatu! Wanashindwa kupata goli hata moja kwa masaa matatu halafu anakuja kutamba hapa.
 
Anasahau msimu wa 2023/2024 walipokuwa wanaamini wakivaa zile jezi zao zenye weusi wanashinda.

Pia juzi kati hapa Haji Manara alisema yeye asipovaa jezi ya Yanga basi Yanga haishindi😀😃😄😆
 
Ndugu mpira ni uwekezaji mambo ya rangi ni unajimu.

Wewe uwe na Aziz k, Pacome, Max, Mzize, Aucho, Chama, Job n. K wawe na utimama mzuri wa akili na Mwili, Bench la Ufundi liloshiba kweli uta anza kuchagua rangi za kuvaa!!!

Ata mkicheza tumbo wazi mtashinda tu, ikitokea kupoteza ni marachache sana.
Tujikite kwenye uwekezaji mambo ya kisayansi hayataki ubashiri.
Walitakiwa Wafunge Goli Moja tu Walishindwa Na Upacome Wao Wote Wakafurushwa Mashindanoni Tofautisha Kati Ya La Familia Na Mpila Wa Kweli.
 
Hao wachezaji uliowataja hapo wanakuzwa Sana ila hakuna kitu. Wote walikuwemo uwanjani wakati Yanga wanashindwa kuifunga MC Alger hata goli moja tu kwa dakika zote 90 za mchezo.
Awa ni wachezaji bora kabisa ila kinachohitajika ni kuongeza wachezaji bora zaidi na mbinu za kisasa zaidi kwakua mafanikio ni mchakato.
Tume toka kwakina Moringa, Ykpe , Ditram n. K tupo hatua nyingine ni swala la mda tu.

Lengo ni kutawala soka la Afrika, kwa apa nyimbani ao nilio wataja ni tishio.
 
Ata mkicheza tumbo wazi mtashinda tu, ikitokea kupoteza ni marachache sana.
Tujikite kwenye uwekezaji mambo ya kisayansi hayataki ubashiri.

Hao wachezaji uliowataja hapo wanakuzwa Sana ila hakuna kitu. Wote walikuwemo uwanjani wakati Yanga wanashindwa kuifunga MC Alger hata goli moja tu kwa dakika zote 90 za mchezo.
Ndugu acha makasiriko yasiyo na maana. Hajasema ukiwa nao haupotezi ila kupoteza inakua ni marachache. Sasa naomba nioneshe timu inayojudge wachezaji kwa mechi moja au mbili.

Wekezeni kwenye ufundi zaidi hayo mambo ni yakizamani achaneni nayo
 
Back
Top Bottom