Simba ilisha wahi kucheza fainali ya kombe la klabu ya mabingwa Caf, uwanja wa chitoholi hukoo Nanjilinji

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Tutegemee kuona habari Kama hiyo baada ya yanga kutinga fainali kutoka kwa wachambuzi nzala/wachambuzi wa mchongo wanaolipwa na Simba sc ili wawatie Moyo mashabiki.

Mwanzo tulikua hatusikii kabisa kuwa Kuna timu ndani ya Tanzania ilishawahi kuingia nusu fainali kimataifa, lakini yanga ilivyotinga nusu zimeibuka "hidden information" kuwa simba walishaga toboa mpaka nusu lakini kabla ya yote hayo wachambuzi/wakaza mishipa ya shingo walikua wakiimba yanga hajawahi kufika robo Ila Simba ndiyo wanashikilia record kwa muda mrefu kwa kufika robo.

Kinachonishangaza hata caf hawajui/ hawana statistics za bwana Yule kutinga nusu fainali na sijui hata kama walivalishwa medani yoyote.

Utabiri wangu ni kwamba yanga akitinga fainali wachambuzi watakuja kuibua data zilizofichwa na CAF kuwa simba alishacheza fainal na al ahly huko chitoholi ili mradi tu kuwapa moyo mashabiki wa simba.

Aliyesema mashabiki wa Simba ni "mbumbumbu" ajengewe sanamu pale Dar es salaam katikati ya mji paitwe "MBUMBUMBU SQUARE"
 
Inashangaza sana kuona wanajitia moyo.
Mashabiki wanahitaji ukweli tu nasio porojoooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…