Robidinyo
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 4,043
- 8,686
Anasema CEO wa Simba, Imani Kajura;
"Timu yetu imeshatoa Bonus zaidi ya Billion 1.1 na kiasi kilichobaki ni milioni 20 pekee tena ni Bonus ya Ligi ya ndani, wewe vuta picha Klabu inalipa zaidi ya Billion 1.1 inashindwaje kulipa milioni 20 haingii akilini hilo ni jambo linalopitia mchakato wa kitaasisi na lipo ndani ya uwezo wetu.
"Vuta picha wachezaji wanalipwa mshahara kiasi gani na ukilinganisha na milioni 20 ambayo watagawana watu zaidi ya 30 kila mmoja atapata kiasi gani, ambapo kukosekana kwake ije iathiri matokeo kwenye mechi,” Imani Kajula Mtendaji Mkuu Simba SC.
Pia Mtendaji Mkuu Iman Kajula, amesema kwenye mikataba yao hakuna sehemu ambayo imesema itawalipa Bonus ila huwa wanatoa kwa ajili ya kuwahamasisha wapambane zaidi kwenye kile wanachokipambania.
Kwa maelezo hayo ya CEO ni wazi, Ahmed Ally nimropokaji kwa uroporopo huu hafai kuwa msemaji wa taasisi kubwa kama Simba.
Jamaa linaropoka maswala ambayo hayapaswi kuropokwa analeta taharuki, linawapa content wachambuzi na mwanya wa kuzusha mambo mengine kutokana na habari alizoropoka.