Simba ilishalipa Tsh. Bilioni 1.1 bonus za wachezaji, inadaiwa Tsh. Milioni 20 tu

Robidinyo

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
4,043
Reaction score
8,686
Anasema CEO wa Simba, Imani Kajura;

"Timu yetu imeshatoa Bonus zaidi ya Billion 1.1 na kiasi kilichobaki ni milioni 20 pekee tena ni Bonus ya Ligi ya ndani, wewe vuta picha Klabu inalipa zaidi ya Billion 1.1 inashindwaje kulipa milioni 20 haingii akilini hilo ni jambo linalopitia mchakato wa kitaasisi na lipo ndani ya uwezo wetu.

"Vuta picha wachezaji wanalipwa mshahara kiasi gani na ukilinganisha na milioni 20 ambayo watagawana watu zaidi ya 30 kila mmoja atapata kiasi gani, ambapo kukosekana kwake ije iathiri matokeo kwenye mechi,” Imani Kajula Mtendaji Mkuu Simba SC.

Pia Mtendaji Mkuu Iman Kajula, amesema kwenye mikataba yao hakuna sehemu ambayo imesema itawalipa Bonus ila huwa wanatoa kwa ajili ya kuwahamasisha wapambane zaidi kwenye kile wanachokipambania.

Kwa maelezo hayo ya CEO ni wazi, Ahmed Ally nimropokaji kwa uroporopo huu hafai kuwa msemaji wa taasisi kubwa kama Simba.

Jamaa linaropoka maswala ambayo hayapaswi kuropokwa analeta taharuki, linawapa content wachambuzi na mwanya wa kuzusha mambo mengine kutokana na habari alizoropoka.

 
Izo unazoleta ni dharau katika makubaliano baina ya timu na wachezaji.

Usitukane watu wanao ongea ukweli, msemaji na wachezaji wanayajua mengi ambayo wewe huyafahamu mkianza kuwadharau na kuwakera watavujisha mambo ambayo yatakuja kuleta taharuki.
Hayo aliyoropoka msemaji tayari yameleta taharuki ndo maana CEO kajitokeza kuyaelezea,.

Kati ya msemaji na CEO nani anaujua ukweli, Huyu msemaji kasema wachezaji wanadai kiasi gani?
 
Hii ndiyo Tanzania. Nilijua hizo mambo zipo kwenye siasa tu.
Kiongozi wa kwanza anasema wachezaji wanadai bonus, huyu mwingine anasema wameshalipwa.
Au basi 🧑‍🦯🧑‍🦯🧑‍🦯🧑‍🦯🧑‍🦯
 
Mbona mnakinzana tena watani
 
Ulipe billion 1.1 alafu million 20 ikushinde unajua hawa watu wameshaona watu ni wajinga sana
 
Makolo dawa ya deni ni kulipa
 

Attachments

  • Kolo.jpeg
    193.6 KB · Views: 2
Tutasikia mengi kisa tu simba wamepoteza mechi
Mi najiuliza kwanini watu hawataki kukubali kuwa kwenye mpira kuna kushinda na kushindwa?wangeshinda haya yote tusingeyasikia
Anafungwa manchester united,sembuse simba?
Mpira wa bongo shughuli pevu
 
asa wale madunduka yanayomsapoti Fei,je madunduka yenu nayo yavunje mkataba???

HAPO NDO MJUE KWANINI YANGA WANAMTIA ADABU BWAMDOGO AWE NA HESHIMA NA MAKUBALIANO PIA IWE FUNDISHO KWA MCHEZAJI ANAYECHEZA TIMU YOYOTE SIO KUDAI DAI VITU AMBAVYO HUSTAHILI THEN WATU WAKUCHEKEE,YANGA WANGEMCHEKEA FEI MANAKE MADUNDUKA YOTE NAYO YANGEVUNJA MIKATABA YAO KWA AJILI YA MASLAHI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…