Simba imepoteza Fear Factor, Itapoteza game nyingi za Ligi kuu

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Fear factor ninile hali ya kuogopwa na timu mbali mbali mara ukutanapo.

Hii factor huzisaidia sana timu kubwa kuweza kupata matokea mazuri ikiwa hata imecheza vibaya sana dhidi ya timu za wastani.

Kitendo cha Simba SC kupoteza mechi 2 kwa idadi ya jumla ya mabao 10 ni kiashiria kikuu kuwa si hata Klabu za nje ya nchi (ambazo zimepoteza hali ya kuogopa klabu hii kutoka Bongo) bali pia hata Klabu za ndani za LigiKUU pia zimenufauka pakubwa kwa takwimu hii

Ninachokiona mbele yangu ni kuwa Baada ya Simba kuanza kushambulia viporo vyao vya ligiKuu, tutaanza kushuhudia sare nyingi sana na hata kupoteza mechi dhidi ya timu ambazo hatutozitarajia.

Hii hali itaeababishwa na kupoteza kwa fear factor yake kwa hata vilabu vya ndani ya nchi. Na patakuwepo na baadhi ya vilabu ndani ya nchi vitakavyodhani kuwa "Kuwafunga Simba kwa bao 3 au 2 ni jambo linalowezekana". Hii itakuwa changamoto kubwa sana kwa Simba.

Itapelekea hata Wanajangwani kutawazwa Mabingwa wa LIGIKUU.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jangwani anasubiri kuangusha point hapo,. hasira zote atazibeba
 
Ni maoni yako, ligi yetu ni dhaifu mno hakuna timu ambayo itaacha kuiheshimu simba Tanzania hata kama ingefungwa magoli 30.
.
Manchester united hata ifungwe 7-0 na Barcelona ikikutana na Chelsea, Liverpool ama Cardiff heshima lazima iwepo.
 
Kama Siku Ile Mbao FC na Simba walifika hatua ya penalty, nakubaliana na wewe kuwa katika Uporo 9,Kuna sare mbili na lose moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
subiri washuke toka misri.... mlengwa namba moja ni mtani tu hatujampopoa na hamsa muda mrefu ila raound hii lazima azinywe
 
Adui namba 1 wa Simba labda awe ni saikolojia yake tu. Vinginevyo timu yoyote itakayoshindwa kuiheshimu Simba ktk ligi kuu itapata tabu sana uwanjani. Ubingwa wa LKB (Ligi Kuu Bara) utaamuliwa na ktk mtanange baina ya watani trh 16 Feb
 
Pia hali hiyo hiyo inaweza kuwasaidia Simba kushinda mechi zake, watakuja hawana wasiwasi wakijua wanafungika kumbe Simba Ni Simba hata kama kalla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…