MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wanalunyasi,
Hali ya timu haihitaji maelezo mengi, ni tatizo lililojikita zaidi kwenye management kuliko level ya technical team na wachezaji. Sasa nawashauri na najua mtasoma hapa.
1) Wanachama waamke sasa, hawa viongozi hawana uwezo wa kufanya mabadiliko yoyote na hata sasa hawajui nini kinatokea. Wanachama waite extra ordinary meeting haraka sana kuweka uongozi mpya.
2) Kama management itabikia hii nawahakikishia Simba iliyojengwa kwa miaka mingi inaenda kubomoka. Daktari hajigangi, hawa viongozi wamepalilia tatizo muda mrefu na sasa tunavuna matokeo.
3) Simba inahitaji mabadiliko makubwa ndani ya siku zisizozidi mbili na kocha mkuu apewe timu ndani ya siku hizo tena akiwa na watu wake wote.
4) Barbara arudishwe haraka na CEO apewe madaraka yote kikamilifu na bodi wabakie na majukumu ya msingi kama reputable organisation zinavyoendeshwa. Kwasasa Imani Kajula anaonekana zaidi kwenye mambo ya biashara lakini mambo ya timu ni kama hausiki nayo sana.
5) Kocha apewe madaraka yote na asiingiliwe kabisa. Apimwe kwa KPI na akipendekeza wachezaji asikilizwe. Management imsaidie pale anapotoa maelekezo ya kinidhamu.
6) Mechi ijayo ni mechi ngumu kuliko hii ya Asec. Kwasasa Simba watoe akili za kufanya biashara kwanza warudishe imani kwa washabiki. Mechi mbili zijazo kusiwe na kiingilio kabisa kama kuwataka radhi mashabiki.
Mwisho, viongozi mliopo mmeangusha sana wapenzi na wanachama. Toka kipigo cha Yanga hii mechi ya tatu timu inafanya vibaya mmeshindwa kuja mbele ya wanachama kuwaomba radhi na kusema mikakati yenu.
Anayeangaika hadharani na timu ni Ahmed Ally huku nyie mkisubiri timu ishinde ndio mjitokeze kunanga waliokuwa wanawazodoa. Kwasababu bado tunawaheshimu iteni press haraka kutuliza wanachama. Mko very slow kwenye maamuzi.
Mashabiki na wanachama wa Simba, ikifika jumatano uongozi haujafanya lolote kimabadiliko ( uzuri mabadiliko ya msingi ni vitu vya wazi) mfahamu tutakuwa kwenye kipindi cha giza hadi wanachama wawatimue hawa viongozi na bahati mbaya huyu kocha mpya tutaenda kuchafua CV yake. Asante