Simba inahitaji viongozi wapya wenye maono mapya!

Tatizo kubwa ni uwekezaji wa mo dewji uliogubikwa na usiri mwingi
 
Kila siku nasema Structure ya Simba inachekesha, waajili watu waache Ubahili wa Kijinga.
Viongozi wa Juu ni wengi kuliko watendaji.
Simba ina Board members 10+....
Baraza la washauri 20+.....
Working Staff ni less than 10......
Hili ni kweli kabisa. Hakuna management paleee ndiyo maana Rais wa Heshima anaweza kubadili bei za tiketi. Siasa zimekuwa nyingi.

Kama sio team itaingia kwenye deni kubwa au mgogoro wa kufikishana mahakamani.
Wazo la mfumo waliotaka kutumia ni zuri sana kama lingetekelezeka shida ni kwamba hakuna uwazi katika uwajibikaji na mipaka ya kazi na pia mifumo ya uchaguzi wa viongozi inayoruhusu rushwa kutembea inavuruga kila kitu.
 
Katiba kumlinda tajiri hilo haliepukiki, hata nchi kila siku tunabadili vifungu vya sheria kuwalinda wawekezaji bila hivyo hakuna mtu atakuja kuweka pesa zake.

Hiyo vita ya tajiri na hao viongozi haiwezi kuisha kirahisi mpaka pale ama tajiri apewe mali yote mazima ili aendeshe timu anavyotaka yeye au aachane na kuingilia masuala ya upande wa pili adili na kile ambacho katiba imempa na wote tunajua tajiri hayupo ok kuwa kwenye nafasi hiyo.
 
Hilo la kwanza halikwepeki sawa

Hili la pili unadhani linatekelezeka ? au kutekelezeka kwake ni mpk watu /mashabiki waumie kwa presha ndio litekelezeke ? Mm sioni muafaka labda warudi Mkutano Mkuu
 
Hilo la kwanza halikwepeki sawa

Hili la pili unadhani linatekelezeka ? au kutekelezeka kwake ni mpk watu /mashabiki waumie kwa presha ndio litekelezeke ? Mm sioni muafaka labda warudi Mkutano Mkuu
Warudi kwa wanachama ila kila upande ukubali kupoteza kitu ambacho ingetamani kukipata
 
Why tajiri anaingilia mambo ya Upande wa Pili? Hata ungekuwa wewe usingekubali hela yako iwe Mikononi mwa Kina Kaburu na Aveva.
Kitu cha Kurekebisha ni kidogo tu, Wanachama waweke end yao ili wapate nguvu na wawe serious.
Board isihusike na Shughuli za Kila siku.
Waajili CEO ambaye ataajiri watu wa kufanya naye kazi.

Sio hii mtu anaweka hela zake afu kihuni tu mnataka kumuondoa. Wakati team ilisha washinda mwanzo.
 
Hivi yule jamaa alie chukua nafasi ya BABRA yuko wapi?
 
Ni mapendekezo mazuri kwa mustakabalili wa 5imba yetu, lakini je tajiri atakubali yote hayo mpaka hayo ya kumnyang'anya uhuru yeye?
Yaani hapo 4 na 5 Kanji mtagombana tu hasa kwenye " kutoa madaraka kamili"
 
Miaka ya Korona walifanya nini cha Ajabu?
Sababu level waliyofika ndiyo ile ile.
Walitumia udhafu ule kupata points za caf na kuwaweka pale walipo sasa,kwa sasa ni ngumu sababu timu nyingi zimejipanga so ili wafikie mafanikio kama yale inabidi wajipange hasa
 
Walitumia udhafu ule kupata points za caf na kuwaweka pale walipo sasa,kwa sasa ni ngumu sababu timu nyingi zimejipanga so ili wafikie mafanikio kama yale inabidi wajipange hasa
Nikisema wewe ni mjinga nakosea?
Msimu Simba anakufa tano tano kulikuwa na Corona?
Mbona alifika Robo?
Msimu uliopita kulikuwa na Corona? Point zilimfikishaje robo msimu uliopita ? Na alianzia hatua ya awali?
Unaweza elezea hili?
 
Unaufahamu mpira angalia Kennedy+Mwenda wamecheza vzr mno kuliko wanaoanza,nilijua anamtoa Baleke na Che malone ili Ngoma arudi nyuma na kumuingiza phiri na Chama hilii kosa walili fanya hata Game ya yanga,play all 3 kanute,mzamiru na Ngoma in 4-3-3 hata lile moja wangelilinda
 
Nikisema wewe ni mjinga nakosea?
Msimu Simba anakufa tano tano kulikuwa na Corona?
Mbona alifika Robo?
Msimu uliopita kulikuwa na Corona? Point zilimfikishaje robo msimu uliopita ? Na alianzia hatua ya awali?
Unaweza elezea hili?
Wewe ndio mjinga,endelea kukariri ukija kushtuka Yanga kishabeba nbc pl back to back miaka 10 mfululizo
 
Pamoja na kuwaheshimu ASEC, lakini Simba haikuhitaji kucheza mpira wa kujilinda kiviiile. Ile mechi kuna watu wakiwemo baadhi ya wachezaji walitaka Simba iipoteze.

Kwa muda mrefu sijaiona Simba inayoweza kukaba na kupambania mipira kama ile ya kipindi cha kwanza ila sijaiona Simba inayopoteza mipira na kulegea kama ile ya kipindi cha pili. Sidhani kama ni issue ya fitness kama wengi wanavyodhani.
 
Me naona tatizo la simba ni mashabiki kuliko uongozi
Mashabiki gani mnataka mashinde tu
This is football
Vipindi vigumu vinakuja na havidumu kuweni na subira
Viongozi wamefanya usajili mkubwa bahati mbaya haukuwalipa
Angalia profile ya ngoma, miquison, kramo, che mallon
Team nyingi hizi nyakati wamepitia
Yanga amejitafuta miaka 4
Tp mazembe wanapitia msoto
Liverpool amekaa miaka 30 bila kombe la epl
Arsenal wamesota
Man u na chelsea wanasota
Lakini mashabiki hawabwabwaji kama mabata ovyo
Tulia trust process nyie mashinde tu ni kina nani
 
Hivi yule jamaa alie chukua nafasi ya BABRA yuko wapi?
Nafikiri anawaza zaidi biashara kuliko management ya team yenyewe. Uto sio rahisi kutokea shida hadi bodi ikimbizane maana wana manage issues zao on daily basis na viongozi wanajua kila kinachoendelea ikiwemo reports za technical team.

Lazima management ihakikishe kila mtu anatimiza wajibu kikamilifu. Mfano unaweza kuuliza CEO taarifa ya kocha wa fitness anaijua au amekaa mara ngapi na kocha mkuu kupata updates juu ya wachezaji na progress ya ufanisi wao? Haya ni mambo ya kila siku lazima mchezaji afuatiliwe!

Una mchezaji kama Onana kwanini kashindwa kuingia first eleven? Management inamfuatiliaje expensive player kama yule kutoonesha improvement? Hata maofisini kila siku lazima ujue nani kafanya nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…