Simba inasalitiwa na viongozi, mashabiki chawa na baadhi ya wanachama wa Dar wanaohongeka

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Simba ya sasa inaongozwa na wahuni ambao wanatumia mtindo wa chama cha siasa kuendelea kubaki madarakani.

Kwanza wametugawa ili watutawale.Baadhi ya wanachama na viongozi hasa wa Dar wanahongwa vipesa ili kuwa upande wa viongozi. Wamebaki na wanachama wazawa wasioenda shule,machawa kina kisugu ambao wanatumika kufanya propaganda ya kulinda maslahi ya viongozi.

Hakuna mkakati wa kusajili wanachama wapya kwa njia za kisasa.Hawa viongozi waswahili kama wataendelea kuwepo,ni bora kuachana kabisa na hii timu kwani huko mbele hali itakuwa mbaya zaidi.

Tumeona mwekezaji bahili na tapeli tu.Anasajili golikipa wa bilioni 3 kumbe tunafanganywa tu ili kesho aje na hesabu zake eti anasaidia Simba na anapata hasara.Kama anapata hasara aondoke timu ianze upya kutafuta mwekezaji mpya.

Imefika wakati tuachane na hawa viongozi wa kisiasa kwani wanasiasa ni waongo,matapeli,vibaka wakubwa wanaojali matumbo yao yasiyoshiba.Wanasiasa ndio sababu ya mauaji yote makubwa unayoyaona duniani
 
Huko sahihi, mwekezaji, viongozi na wanachama machawa ndio tatizo kubwa na hawataki wanachama wapya waongezeke. Hawa ndio walichagua viongozi kwa kuletewa Manzoki. Wanajali maslahi yao kuliko ya timu labda tukiwachapa bakora akili zitawarudi.
 
Halafu machawa wa viongozi simba ni vijana kabisa ,mpk unajiuliza huyu kijana anakuaje chawa ktk ujinga km huu ?
 
Mashabiki wa Simba Hamna akili
 
Mangungu kabla ya uenyekiti alikuwa nani pale Simba?
 
Mangungu kabla ya uenyekiti alikuwa nani pale Simba?
Mangungu mtoto wa mjini, anakaa Libya street, mtapiga kelele za mitandaoni tu lakini hamumuwezi.

Muombeeni 2025 arudi kwenye ubunge ndio Salama yenu.
 
Mangungu mtoto wa mjini, anakaa Libya street, mtapiga kelele za mitandaoni tu lakini hamumuwezi.

Muombeeni 2025 arudi kwenye ubunge ndio Salama yenu.
Eng Hersi kabla ya uraisi alikuwa amesimamia mambo kadhaa pale akaprove
 
Msifanye masihala kumshawishi kiongozi wa FIFA mpaka kugeuza shingo na kumwangalia kiongozi wa Simb na kumsifia, sio kazi ndogo rais katumia nguvu nyingi sana kugeuza shingo na tuzo mkapewa. Hamuoni kuwa hayo ni mafanikio ya viongozi wenu,ambao waliwaletea Manzoki kama msimamizi wa uchaguzi.
 
Huko sahihi, mwekezaji, viongozi na wanachama machawa ndio tatizo kubwa na hawataki wanachama wapya waongezeke. Hawa ndio walichagua viongozi kwa kuletewa Manzoki. Wanajali maslahi yao kuliko ya timu labda tukiwachapa bakora akili zitawarudi.
Huko sahihi ❌️❌️❌️
Uko sahihi ✅️✅️✅️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…