Simba inavyozama sasa una chochote cha kuwashauri?

Hiyo Simba iliyoshuka ndio hii ambayo haijapoteza mchezo wowote na ndio iliyofungwa magoli machache hadi sasa au kuna Simba ingine huko kwenu Kimanzichana?
 
Mm ni Simba Ila Yanga wana timu ya moto sana na msimu huu wala hatuwawezi kabisa
Kweli mwana Simba mwenzangu hata mimi naona Hawa Yanga wana timu haswa mwaka huu sisi Simba hatuna chetu tujipange kwa ajili ya msimu ujao
 
Usicho elewa ni kuwa, YANGA msimu Uliopita Walikuwa na Timu Mbovu kiasi kwamba Mchezaji Yeyote Watakaye Msajiri alikuwa na uhakika wa kuingia kwenye kikosi cha Kwanza na Kupata Namba ya Uhakika, Hakukua na Cha kupoteza kwasababu Timu ilikuwa mbovu, Ndio maana Wachezaji wote walio sajiriwa Yanga Walipata namba. Sasa Ulisha wahi jiuliza sahizi Yanga Ikitokea Wana Majeruhi kama Ya Simba Timu Yao itakuwaje? Tuseme wachezaji 3 wa Yanga Wapate majeruhi Umeshajiuliza Timu itakuwaje?

Simba Msimu uliopita walikuwa na Kikosi Bora, kikosi kile kile kimekuja msimu huu huku Chama na Luis wakiondoka, Wakasajiri wachezaji wapya ambao wanahitaji Ku fight kupata Namba Pale Simba, Kwa kikosi Cha Simba Sio Rahisi kuja Kuingia na Kupata Namba Kirahisi kulingana na Ubora wa Kikosi walio ukuta. Kibu Denis kapata bahati kwasababu kafika Mugalu akiwa majeruhi, Bila hivyo naye Angesugua Bench kufight kupata Namba. Kanoute kapata Namba kirahisi kwasababu Chama Hayupo, wengine walio Baki wanahitaji Kupambana Kikosini, Simba Imepata wachezaji wengi majeraha lakini bado wako vile vile….. na simba Majeraha huwa yanawasumbua mwanzo wa Msimu baada ya Hapo gari huwa limewaka.

Yanga Sahizi Watababweteka Hawatutumia nguvu kusajiri, lakini Tunavo enda Mzunguko wa pili, Utaona Wachezaji walivyochoka wakati simba Inakuwa na wachezaji wengi wa Machaguo, Ndio maana Sahizi mchezaji simba Atapata majeraha na Benchi la Ufundi linaweza Lisiwaze chochote kwasbabu Kocha anafanya Rotation nzuri ya wachezaji na Taratibu wanaanza kuingia kwenye Mfumo.

Yule Sakho na Banda wakichukua Namba Simba Hamna Mchezaji wa Yanga wa Kuwafikia, Mchezaji kama Duncan Akichukua namba Yule hakuna wa kumzuia… angalia HD alivyopambana…. Sasa Yanga Huwezi kutegema Mayele na Jesus msimu ujao Kuwa Na Viwango hivi kwasababu Wanatumika sanaaaa yaani kifupi ni Kauka ni Kuvae

Usajiri ni Hesababu na Sayansi Nzuri sanaaa, Simba Haikuwa inahitaji matokeo ya Haraka katika sajiri zake lakini Yanga ni kama Uajiriwa kwenda Kuziba Nafasi ya Marehemu yaani Hupewi hata Orientation wewe unafikia Kazi kazi

Wait and See Msimu huu mwishoni
 
Itabidi waiprint hii wakasomeane na kuiweka ukutani kwa marejeo.
 
Siyo mwana simba na hutuingizi mtegoni...unamtaja Dennis Nkane unamcopare na Wawa na Bocco..why usizungumzie Banda na Sakho..then tangu dirisha lifunguliwe Simba hatujatangaza mtu Kama mwana Simba kweli why usivute subira ujue nani anakuja?..cha kukwambia tu Yanga ni wazuri ukilinganisha na walivyokuwa wao wenyewe kwa misimu minne nyuma Ila si kwa kuilinganisha na Simba..timu nzur na sisi wabovu hadi sasa gape ni point 2..timu nzur mechi na Namungo ilikuwa tia maji tia maji..timu nzur klabu bingwa kapigwa nje ndaniii mchana kweupeee..acheni Porojo Yanga mateso yapo pale pale kuongozaga ligi ni kawaida yenu
 
Yanga huyo kaka..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…