Simba inaweza kutolewa klabu bingwa leo, Historia ina tabia ya kujirudia.

Mr Alpha

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
273
Reaction score
765
Kama umefuatilia mechi za simba karibuni utagundua timu imekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa siku moja barabarani wiki gereji

Timu haina kikosi aggressive chenye uchu wa mabao na muunganiko wa ushindi, timu imekuwa ikipata matokeo ya papatu papatu kulingana na siku

Simba kocha wanae mzuri shida kubwa ipo kwenye wachezaji, ina wachezaji wa kiwango cha chini mno hususan eneo la ushambuliaji likiongozwa na mchoyo na mbinafsi namba moja Saido Ntibazonkiza akisaidiwa na mzee wa makamo Clatous Chama (huyu ameisha kiwango amebaki jina tu japo kolokwinyo wengi hawataki kuamini kabisa)

Leo sitashangaa Jwaneng Galaxy wakipeleka kilio kizito mitaa ya Msimbazi, Jwaneng nao ni kama simba hivyo hii mechi ya leo ni kama mechi dhidi ya pwagu na pwaguzi lolote laweza kutokea leo

Tuwaombee kwakweli
 
Simba inashinda, zaidi ya magoli mawili.
Kuna penati ya Saido na goli lingine litafungwa kawaida na mchezaji kutoka Cameroon. Na pia kuna uwezekano Jwaneng wakajifunga la tatu. Tupo Bagamoyo hapa tunachungulia mchezo utakavyokuwa.
 
Kuna watu wataumia sana mambo yakie da tofauti na ulivyosema ndugu mtabiri.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…