Simba inazidi kutumbukia shimoni, kumbe hata simba day wanalipia promo..!

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu.
Naumizwa sana na klabu kubwa namba moja africa yenye mataji lukuki ya kimataifa ikiwemo CAFCL. Kuzidi kuporomoka namna hii na kukosa ushawishi kabisa kwanzia uwanjani mpaka nje ya uwanja..!

Majuzi kwenye kipindi cha michezo wasafi kuna msikilizaji aliuliza " "mbona mnapigia promo sana simba day pekee vipi kuhusu week ya mwananchi?"

Kwa hamaki ndipo yule mtangazaji akajibu "hii ni biashara wamelipia tusiharibiane biashara"

Sasa nimegundua tofauti.
Yanga wao kuelekea tamasha lao kesho hawajalipia sana promo redioni wala kwenye TV's. Bali wameenda kisasa zaidi kwa kuhamasisha mitandaoni na kwa kuwa wana mashabiki wengi zaidi basi hata wasipofanya promo tamasha litajaa na kufana sana na hii ndiyo maana ya team kubwa,

Ukiachana na hilo la kumleta kocha fundi pitso mosimane kitu ambacho simba wanajinasibu wakubwa hawawezi zaidi ya kuwaleta kina zuchu na wale st George...

Hapa imeonekana wazi team gani hasa ni kubwa na yenye mashabiki wengi licha ya simba kufanya promo kutwa kucha na kusaini mkataba na clouds kabisa lakini hawatojaza uwanja na wengi wataokuja ni wale mashabiki wa yanga kuja kuona vituko basi..

Simba inazidi kutumbukia shimoni kabisa na viongozi wasipoliona hili basi msimu huu watagombea nafasi na kina singida big stars..!

Team mpaka sasa inapiga kalenda kila siku kuhusu jezi mpya zinatoka lini? Nk Madudu na viongozi waliojaa hapo ni wafunga vikao na wafungua vikao kama alivyo yule jamaa mropokaji (mangungu)

Iokoeni simba wajameni yetu wajameni sisi mashabiki ndio tunaoumia..
 
Toa pumba zako hapa.
 

‘Hawajalipia sana promo’
Ficha ujinga wako kdg
 
[emoji706]
 

Umeandika kama unakufa. Kinachokuuma ni strategy za simba kuelekea simba day au ni kutokufanya kama Yanga? Maana kama hoja ni kwamba simba inafeli kufanya promo kuelekea simba day mbona ume compare na Yanga ? Ungefanya critical analysis kwenye statrgey za simba kuelekea simba day na siyo kusema Yanga kafanya hivi au vile.

Swala LA mashabiki liko wazi siku zote Yanga ana mashabiki wengi hii inaonekana kwenye takwimu za mapato ya uwanjani .
 
Yanga wenye akili ni mheshimiwa kikwete na Baba yangu(manara,2021)
 
Kweli ukitoa wale wawili, waliobakia wote manara keshajisemea.
 
Umetype ujinga
 
Umekaa chini na kinyesi halafu unajiona umeongea point,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…