HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Leo tarehe 19 Simba anacheza na Ndanda, keshokutwa tarehe 21 Simba anacheza na Singida United na tarehe 23 Simba anacheza na Sevilla. Tukumbuke hakuna shirika la ndege linaloenda Singida, wala hakuna uwanja wa ndege mkubwa ambapo Simba ingeweza kukodi Ndege, hivyo usafiri pekee ni basi ambapo Dar hadi Singida ni km 718. Usafiri wa basi ukizingatia torch na speed limit ya 80 km kwa saa pamoja na chakula njiani na kuchimba dawa ni masaa 11. Hivyo kama Simba wataondoka kesho alfajiri saa 10 watafika Singida kesho alasiri saa 9. Hivyo watapumzika tu bila kufanya mazoezi kusubiri mechi ya keshokutwa na baadaye usiku kuanza safari ya kurejea Dar ambapo watafika mchana wa tarehe 22 siku ya Jumatano na Alhamisi watacheza na Sevilla.
Ni dhahiri wachezaji watakuwa wamechoka kupindukia na hawatakuwa katika kiwango cha kupambana na timu kubwa ya Hispania, itakuwa aibu.
Nashauri Simba kikosi cha wachezaji wa akiba kule Singida, na 11 bora wabaki kuisubiri Sevilla. Kama ni ubingwa Simba ataupata tu kwa msimamo ulivyo. Ubaya zaidi Simba sasa hivi imepungukiwa na wachezaji kwani kuna majeruhi hasa mabeki kama Juuko, Bukaba na Kapombe. Ingawaje taarifa nzuri ni kurejea kwa Wawa.
11 bora wa kubaki na Aussems 1. Manulla 2. Gyan 3. Tshabalala 4. Nyoni 5. Mpilipili 6. Mkude 7. Niyonzima 8. Chama 9. Bocco 10. Kagere 11. Okwi
11 wa akiba kwenda na kocha msaidizi Singida 1. Dida 2. Zana 3. Kwasi 4. Kotei 5.Wawa 6. Ndemla 7. Abdul Hamisi 8. Muzamiru 9. Salamba 10. Mo 11. Dilunga Reserves Ally Salim, Vincent Costa na wengine under 20