Simba isimuache Saido Ntibazonkiza bado ana mchango mkubwa sana

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Saido tangu ajiunge simba akitokea Geita amekuwa na mchango mkubwa sana, ndiye mchezaji pekee ambaye kila msimu katika idadi ya wafungaji mabao hakosi tatu bora, ndiye mchezaji anayejua kupiga penati kuliko wachezaji wote nchini, kwake penati ni goli la bure, amewaonea sana makipa.

Saido bado ana nguvu, kipindi hiki Simba imevamiwa sana na mashabiki andazi na wajinga wajinva wengi, cjui hata wametokea wapi hakyamungu.

Ukiwauliza kama wanamjua Jimmy David Ngonya hawamjui, hawamjui Ally Amir Bamchawi wala Juma Salum, wala Priva Mtema, wala Halfan Matumla wala nani.

Hawamjui Malota Soma wala Twaha Hamidu, wala Rafael Paulo wala Iddi seleman wala Ally Machela.

Hawa wanatusumbua sana na wanapenda sana waonekane social media.

Wamemkatisha tamaa Saido akawa kila akifunga hana furaha, anaishia kuwawekea kidole mdomoni.

Saido ni muungwana sana, ana uzoefu wa kutosha, ana nguvu za kutosha, maarifa ya kutosha, akili za kutosha, hekima na busara.

Ndiye mchezaji ambaye hakuna kocha aliyepita Simba akamweka benchi mwanaume huyu mcha mungu.

Huyu kwa timu inayohitaji mafanikio anastahili kubakia, umri ni namba tu lakn mwanaume huyu ni mkatili sana kwa mabeki na makipa.

Timu yetu haina umoja, imejaa usaliti mwingi mno, majungu, fitna na kila aina, walioko madarakani wanaonekana wameingia kwa hila hivyo walioshindwa wamepambana sana kuhakikisha hawafanikiwi.Kila wakipanga wao wanapangua.Wakaamua kabisa kuchomesha tupigwe matano na Yanga ili uongozi uonekane hauna uwezo.

Wamemtumia sana zungu pori kuihujumu timu yetu.

Zungu pori ndio kiungo baina ya kijana na nyekundu.

Zungu pori amepewa kitengo kabisa cha kucheza na timu yetu, akififisha mipango yote ndani ya klabu.

Hata msimu ujao hatutaweza kufanikiwa kama wataendelea hawa hawa wanaohujumiwa.

Saido ni asset sema watu wa mpira hatuna tena, hasara tupu
 
Sawa, ila Coastal union Saidoo atashine zaidi , huku Simba anapendeza tu nafasi ya tatu
 

Attachments

  • sokavibe6_1717060562453222.mp4
    3.3 MB

Naungo Mkono hoja Yako!
Ila Naomba kuboresha yafuatayo:
Tatizo la Simba ni Kumtegema Mchezaji
simba Inatakiwa kuwa na Kina Saido kama 2
kwa hiyo kuwa na Mbafsla wa Kila Mchezaji na Sio kutegemea Mchezaji Mmoja!
Watafute Mwingine kama Saido! Yaani wawe na Washambuliaji kadhaa mabeki kadhaa ambao akikosekana huyu yule anaziba!
Saidoo anaweza baki ila Akawepo na Mwingine hii itasaidia Sanaa Katika Kuwatumia wachezaji!
haswa nyakati Muhimu!
Saidoo huwa anaonekana wakati muhimu!
Hivyo Simba wanatakiwa wawe na Mbadala yaani awepo saido na Mwingine!
 
Mimi sielewi kwanini wanasimba wana chuki kali dhidi ya Saidoo. Saidoo ndiye mfungaji bora msimu uliopota akiwa na Mayele, saidoo ndiye mfungaji bora wa simba msimu huu. Saidòo ni mchezaji mwenye kujituma sana. Why saidoo? Vipenzi vyenu kina chama na kibu wamefanya nini cha kujivunia msimu huu? Why matusi kwa saidoo? Hii si busara kwa soka la Tz
 
We kweli umepitwa na mda saidoo kwenye mkataba wake kuna kipengele cha yeye kucheza mechi kwa dakika 75 akiwa fit na sio kwamba wanamuanzisha kwa uwezo wake mchezaji mbinafsi kama yule wa nn simba sehemu ya kutoa pasi anataka kufunga halafu kila faulu anataka apige yeye aondoke kama sio ubinafsi wake simba isingeenda shirikisho.
 

".... mwanaume huyu mcha mungu"

Wadada mkipenda mnapenda kweli kweli.
 

Usimshangae wanawake huwa wanaendeshwa na mihemko sana.
 
Kumbe majini mnayajua?
 
Kampamba sana ila saido ni Moja ya wachezaji arrogant sana nakumbuka akiwa yanga aliwahi kutoka uwanjani kwa dharau baada ya kufunga kocha akaanza kumbembeleza arudi uwanjani ilikuwa fedheha sana kwa kocha
 
Ukiondoa magoli yake Simba ingekua nafasi ya tano
 
Msimu wa usajili umeshafika machawa wa Saidoo wameshaanza kazi na wamejipanga kweli kweli. Kati ya wachezaji waliyeifelisha Simba msimu huu mmojawapo ni huyo Saidoo. Na kwa jinsi machawa walivyojipanga na kwa kuwa Mangungu na Try Again hawaujui mpira vizuri ila ni wajanja wajanja kwenye mambo fulani hapa lazima wajae na Saidoo kupewa mkataba mwingine haitakuwa jambo la ajabu hasa ikizingatiwa hana ubishi wa kutoa 10%. Ndio maana Phiri na Chama kila siku walikuwa wanaonekana wakorofi kwa sababu kupinga kutoa 10%. Mwisho wa siku Phiri akawa mbuzi wa kafara lakini Chama ikashindikana kwa sababu yupo mioyoni mwa wanasimba wote na viongozi wanajua wazi wakilazimsha kumtimua Chama basi wataondoka wao viongozi.

Ni ujanja tu unatumika hapa unawaondoa Baleke na Phiri kwa njia yoyote ile unaleta magalasa Freddy na Jobe matokeo yake Saidoo anaonekane kama mchezaji wa kutumainiwa Simba ili kutengeneza mazingira mazuri ya kusajiliwa tena. Wenye akili na wanaojuwa mpira ndio wataelewa namna gani viongozi wanavyopiga pesa za Simba hapa kupitia Saidoo.

Saidoo ni mchezaji mbinafsi anayetaka kufunga mwenyewe hata sehemu ya kuwapasia wenzake wafunge, kila mechi anaanguka mwenyewe zaidi ya mara kumi uwanjani na zaidi ya mara tano anaposukumwa na wapinzani, katika nafasi tano anafunga mara moja tena kama sio kwa faulo basi ujue ni penati na kila mpira wa faulo hata kama sio upande anaoweza kufunga kutokana na mguu wake anataka apige yeye, analazimisha kupiga chenga wakati umri umeenda akili inataka mwili hautaki matokeo yake anapoteza mpira na mipira mingi huwa inafia kwake hivyo kuinyima Simba magoli, n.k.

Kwa Simba hii ya Mangungu, Kajula na Try Again inayotaka kubeba kombe la muungano "back to back" napendekeza impe mkataba mpya Saidoo tena haraka sana na atawafaa na kuwasaidia sana. Lakini kwa Simba aliyokuwa anizungumzia Mo siku zilizopita yenye ndoto za kufika fainali ya Afrika na kubeba kombe la Afrika huyo Saidoo wenu hafai hata kidogo. Ni bora mara mia moja Simba ikawekeza kwa Chasambi na kuachana na huyo mzee Saidoo akalee wajukuu.

Hivi machawa wa Saidoo na viongozi wa Simba wameshajiuliza iwapo Baleke na Phiri wangekuwepo kwenye mzunguuko wa pili wa ligi wangemaliza wakiwa na goli ngapi kila mmoja? Je Simba ingehangaika kutafuta nafasi ya pili na kuikosa? Mimi naamini kabisa Baleke na Phiri wangekuwepo Simba mpaka mwishoni mwa msimu Simba ingeweza hata kubeba ubingwa mwaka huu.

Ni mtizamo tu
 
[emoji1787][emoji1787] huyu jamaa itakua kuna mda zinafyatuka na kuna mda zinakaa sawa
 
Kampamba sana ila saido ni Moja ya wachezaji arrogant sana nakumbuka akiwa yanga aliwahi kutoka uwanjani kwa dharau baada ya kufunga kocha akaanza kumbembeleza arudi uwanjani ilikuwa fedheha sana kwa kocha
Wenzako wanasema ni mchezaji professional kacheza ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…