Simba isiposhinda Derby ya tarehe 19 itakuwa ni uzembe mkubwa sana kwao

vibertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2022
Posts
2,474
Reaction score
4,726
Kuelekea mechi ya tarehe 19, timu ya Simba ina advantage kubwa sana kutokana na kuwa na idadi ndogo sana ya wachezaji walioitwa kwenye mataifa yao. Kuitwa kwa wachezaji wengi kwa upande wa Yanga kuna athari ya mwalimu kushindwa kupanga program zake za kimbinu na kiufundi kuelekea kwenye mchezo husika. Tarehe 15 ndio timu nyingi zinakamilisha mzunguko wa 4 kufuzu AFCON, hivyo wachezaji wataanza kusafiri kati ya tarehe 16 hadi tarehe 17 huku kukiwa na siku moja tu ya maandalizi kuelekea kwenye derby.

Ukiachana na sababu ya kocha kushindwa kupata muda wa kutosha kuandaa program yake, jambo la pili ni fatigue. Wachezaji wa Yanga watakuwa kwenye uchovu kutokana na kutoka kucheza mechi karibu karibu na pia uchovu wa safari. Hawatokuwa na muda wa kupumzika.

Wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye majukumu ya mataifa yao na wamecheza mechi ni
1) Diara
2) Aziz Ki
3) Chama
4) Abuya
5) Dube
6) Musonda
7)Bacca
8)Job
9)Mzize
10) Mudathir
11) Aucho

Hawa ni wachezaji wanaounda kikosi cha kwanza cha Yanga kwa asilimia kubwa, na ndio wanaokosa kushiriki katika mpango kazi wa Gamondi kwa asilimia 100 kutokana na muda. Hivyo Simba mshindwe wenyewe kushinda siku ya jumamosi favour ipo upande wake.
 
Good thinking
 
Ni humu tu 😎 Mwendo wa mabarafu mpaka kieleweke, Aziz ki akirudi tu hatoki humu mpaka siki ya derby 😀 YANGA BINGWA
images - 2024-10-15T133010.150.jpeg
 
Ukiwa na timu au wachezaji wazuri,huitaji sijui muunganiko sijui program, sijui wachezaji hawajazoea, izo sababu ni ishara Hauna wachezaji au timu,, ukiwa na wachezaji wazuri mnapgiana simu tu na anapigwa mtu
 
Kitakacho Fanya Simba wafungwe ni ubora wa wachezaji tu.
Yanga Ina timu imara Sana.
 
Back
Top Bottom