Themann
JF-Expert Member
- Apr 15, 2022
- 3,842
- 16,058
Ndugu zangu mashabiki wa simba sc hawa watu wawili ndio wanaididimiza simba tunahitaji twende mbele ila tunarudi zaidi nyuma ukiangalia simba ndio imefanya ligi ya tanzania itambulike kwa 80%huko duniani sasa kadri siku zinavyozidi kwenda tunarudi nyuma zaidi na wenzetu upande wa pili naona wanapiga hatua kubwa zaidi…
Tuangalie ndani ya msimu mmoja wameweza
Kufika fainali ya shirikisho sisi miaka nenda rudi tuko pale pale hii yote inachangiwa na
Sajiri za mafungu na za show off hizo zama Zilishapitwa na wakati.
Timu yetu inawachezaji wazee tukubali hilo Hii inachangiwa na hawa watu wawili mangungu na mwenzake kipindi cha uchaguzi alifanya danganya toto ya kumleta manzoki ili tu apite katika nafasi aliyopo sasa
Baada ya kupita manzoki naye akasepa huyu ni tapeli mohamed dewji
Tunahitaji hawa watu wawili wang’olewe..
Katika nafasi hizi tusipo angalia simba ubingwa tutauskia midomoni mwa watu.
Ni wakati pia wakupitisha fagio la wachezaji wazee wote acheni kuendesha timu kimazoea ligi na soka la tanzania limebadirika kila timu inasajiri vizuri kushindana na timu hizi mbili kubwa
Akumbukwe hans pope.