Simba: Kocha Gomez anasoma online course, tuna imani hadi mchezo wetu unachezwa atakuwa ameshamaliza masomo

Simba: Kocha Gomez anasoma online course, tuna imani hadi mchezo wetu unachezwa atakuwa ameshamaliza masomo

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kumtaja kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes kukosa sifa za kukaa benchi la ufundi la Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kutokana na kukosa sifa, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kutolea ufafanuzi.

Gomes ana (UEFA A Diploma) na kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho hilo wanahitaji kocha awe na CAF A au UEFA PRO LICENCE.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu alisema ujio wa taarifa hiyo kwao si mpya kwani tayari kocha wao alishaanza kusoma.

"Hatujashtushwa na taarifa hizo kwani ni muda tu tulitaarifiwa na kocha akachukua maamuzi ya kusoma kwa njia ya mtandao (online) tuna imani hadi mchezo wetu unachezwa kocha atakuwa ameshamaliza masomo," anasema.
 
Issue sio kusoma online, Je anaweza kufaulu mitihani akayopewa na CAF hadi kupata cheti chake
Anaonekana mtu ambaye kichwa chake ni kigumu kuelewa mafundisho
[emoji1787][emoji1787]anaonekana hawezi kuelewa mafundisho..utadhani wewe ni mwalimu wake

Utopolo Yule msukule ghafla kawaambukiza maneno ya kuudhi yani
 
Hivi hiyo ya kusoma online si ndo ile enzi za wazazi wetu walikuwa wanasema kusoma kwa njia ya posta?!
 
emoji1787.png
emoji1787.png
anaonekana hawezi kuelewa mafundisho..utadhani wewe ni mwalimu wake

Utopolo Yule msukule ghafla kawaambukiza maneno ya kuudhi yani
Hahaha kwamba mkuu hauna taarifa kwamba Thierry Hitimana anakuja kuwa msaidizi pale wa Da Rosa ili ikifika wakati champions league Hitimana ndo anasimama kwenye bench

Na hii inathibitisha Da Rosa ni kocha wa Chandimu
 
Hivi niulze kina lampard,sosha, Gerald wao walisoma kbla ya kuwa makocha au ndo Europe hakuna hyo sheria
 
Jamaa wa makolo kumbe kocha wenu ngumbaru?
Ngumbaru FC sisikii tena zile kelele za tupo nafasi ya 12😀😀😀
 
Hivi niulze kina lampard,sosha, Gerald wao walisoma kbla ya kuwa makocha au ndo Europe hakuna hyo sheria
kweli makolo ni matahira 😀😀
Wenzio kule hakuna upiga dili kama kwa mudi
Lampard ni mmoja ya wachezaji wasomi
Unafananisha na ngumbaru wenu?
 
Back
Top Bottom