Simba kuishangilia Yanga kwa masharti

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Dar es Salaam.

Klabu ya Simba imewapa masharti mahasimu wao wa jadi, Yanga kama inahitaji mashabiki wao waishangilie kwenye mchezo wa keshokutwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), dhidi ya BDF IX ya Botswana.

Simba ilieleza jana kuwa katika mchezo huo, mashabiki wake wataingia uwanjani wakitanguliza utaifa kwanza, lakini kwa sharti la Yanga kutowaangusha na kucheza mpira wenye kiwango, kinyume na hapo watabadilika na kuelekeza nguvu zao kwa wapinzani, BDF.

Rais wa Simba, Evance Aveva aliliambia gazeti hili jana kuwa katika mchezo huo watakuwa upande wa Yanga iwapo watacheza mpira wenye kiwango kama ule unaochezwa nao (Simba), tofauti na hivyo watawageuka katikati ya mchezo.

"Kwenye mechi hiyo tutatanguliza utaifa kwanza kwa kuiunga mkono Yanga mwanzoni mwa mchezo na tutaendelea kufanya hivyo hadi mwisho, kinyume chake tutawageuka.

"Ingawa haijawahi kutokea Simba ikaishangilia Yanga, lakini kwenye mchezo huu tumeamua kutanguliza mbele utaifa, lakini tukiona Yanga ‘wanambwelambwela' (hawaeleweki) uwanjani kwa kucheza chini ya kiwango tutawabadilikia na tutaiunga mkono BDF," alisema Aveva na kuongeza:

"Tutafanya hivyo kwa kuwa timu inayoshangiliwa ni ile inayocheza mpira safi, wenye kiwango, hivyo watani zetu wasipotuangusha, sisi tutawashangilia, lakini ‘wakizingua' (wakikorofisha), tunawabadilikia na kuwashangilia wageni (BDF)."

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alipoulizwa kuhusu azma hiyo ya Simba, alisema wamepokea kwa mikono miwili uamuzi huo wa kuwashangilia.

"Tunafurahi kwa uzalendo wao, tupo tayari kutoa tiketi za bure kuingia uwanjani, pia kama mwakani watafanikiwa kufuzu kucheza mashindano ya kimataifa nasi tutawashangilia," alisema Muro.

Wakati huohuo, kocha wa Yanga, Hans Pluijm ameongeza dozi ya mazoezi kwa wachezaji wake, hasa safu ya uhambuliaji na kiungo kuelekea kwenye mchezo huo wa Jumamosi.

Pluijm ameikomalia safu yake ya ushambuliaji na viungo kwenye mazoezi yanayofanyika asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku akibainisha kuwa hana wasiwasi na safu yake ya ulinzi.

"Nahitaji mabao mengi kwenye mechi ya nyumbani. Hii ndiyo itatupa nafasi nzuri hata tutakapokwenda kucheza mechi ya marudiano ugenini, sitaki timu itengeneze nafasi nyingi na kufunga moja au mbili.

"Ninachohitaji ni kuwa tukitengeneza nafasi 20, tuzitumie zote, ikishindikana magoli yapatikane kwenye nusu ya nafasi zote tulizotengeneza, sihitaji magoli machache, nimelifanyia kazi hilo na sasa mambo yanakwenda vizuri," alisema kocha huyo.

Mwananchi
 
Yaani sisi timu ya wananchi tucheze kiwango kama cha simba ambao wako nafasi ha mkia ni wa ligi ndo watushangilie?
 
Yaani sisi timu ya wananchi tucheze kiwango kama cha simba ambao wako nafasi ya mkiani mwa ligi ndo watushangilie? Tuwaige wao tiwe nafasi ya chini? No never, yanga moto bati pigieni soka kiwango msiige mchezo wa simba wa madroo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…