Simba kumkataa Manara sijaona kama imekaa poa

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Uongozi wa Simba kulingana na taarifa zilizotolewa na Haji Manara ambaye ni Mkuu na Mkuu wa habari wa habari mbele ya mechi yao dhidi ya Plateau United jambo hili halijakaa poa. Wangetafuta namna ya kuona sawa na kusawazisha lakini sio kumkataa kwa sababu siamini kama Manara ametoka tu nyumbani alifanya wanahabari akaongea.

Naamini alikuwa na baraka zote za klabu ndio maana alikuwa na Kaimu Mwenyekiti Mwina Kaduguda. Kama imetokea ameteleza, inatakiwa klabu itoea taarifa ya kufafanua na kuona sawa na msimamo wa klabu juu ya jambo fulani lakini sio kumkataa moja kwa moja.

Jambo hili linatazama katika kiwango cha kitaasisi na Manara alikuwa anaiwakilisha taasisi. Mimi naamini Simba ilimtuma Manara mavazi na wanahabari kwa lengo la kuamsha mechi ya Jumamosi kutokana na alivyojijengea umahiri katika eneo hilo.

Mwisho wa siku hakuna mtu anaezuiwa kwenda uwanjani, viwanjani sisi tunahamasisha amani, kweli, watu kushangilia na kuzodoana kupo lakini sio hatua hatua ya kutengeneza chuki na uadui.

 
Mashabiki wa Yanga na wakae nje tu aisee, nikikumbuka walivyowashangilia AS Vita ile mechi ya robo fainali na bahati nzuri Simba ikafanikiwa kutupa nje, sasa ni wa kazi gani mashabiki wa kuja kuwapa support timu pinzani tena kutoka nje ya nchi yetu?

Hivi mafanikio ya hiyo timu ya nje ya nchi yetu yana maslahi gani na nchi yetu?
 
Kuna umuhimu mkubwa kwa Yanga kuishangilia Simba kuliko kuizomea.TFF kwa hili hawako sawa,wapi Real Madrid ikicheza na Ac Milan washabiki wa Bacelona waingie na jezi zao kuwazomea Madrid. Huu ni utani wakijinga kabisa.
 
Ismail Aden Rage hakukosea kabisa kuipa jina linaloistahili hii club - Mbumbumbu SC!
 
Manara yupo sahihi tu. Alihamasisha mashabiki wa Simba ndio wawe wengi uwanjani, CAF imeruhusu idadi ya watu waingie nusu. Kuna haja gani ya kuacha mamluki waende uwanjani wakati tunaohitajika kutoa hamasa tupo.

Tumeshuhudia wanachokifanya wapenzi wa Yanga wanavyowachania jezi nyekundu kwenye mechi zao kwa nini sisi tusiwageuzie kibao?
 
Huyu manara akili Hana kabisa na atakuja kuleta balaa siku moja TFF wawaangalie hawa wasemaji wa hizi timu.
 
Haji Manara ni sikio la kufa, upinzani wa Simba na Yanga upo na utaendelea kuwepo kwa miaka mingi anacho kitengeneza Manara ni chuki baina ya Simba na Yanga. Muda si mrefu yeye mwenyewe au mpira wa Tanzania utakwenda kuvuna chuki inayo pandwa.
 
Mtani naona na wewe unamkataa Msemaji wenu. Lol

Nilimkataa toka mwanzo, ni ujuha kujipa mamlaka ya kusema eti nani aingie na nani asiingie, ile ni for public consumption.

Labda anunue tickets zote 30,000 awagawie anaotaka waingie, ila si kutoa tamko la kuzuia washabiki wa Yanga.

BTW, Yanga hawaja shiriki Klabu Bingwa, waache waje wainjoi ushiriki kwa kuangalia kaka zao Simba wanavyo wawakilisha. Kwa nini tuwanyime wenzetu kuona pira biriani likitandazwa na kuwaondoa wa Nigeria!
 
Tangia muda anaanza kujiroposha roposha kuhusu ukumbi kuchafuliwa na viongozi wa Yanga nikajua lazima atanogewa na kuharibu mambo.

Pole yake japo huwa namuona kama sikio la kufa ambalo saa nyingi linajali hisia za followers wake huko Insta.
 
Hayo ndiyo matatizo ya kuweka vilaza kwenye nafasi ya usemaji
 
Mimi ni mwanasimba haswaa,uongozi umefanya vzr kumkataa hadharani.

Tatizo Manara ni mropokaji sana.
ubaguzi una gharama kubwa ya kulipa tusisahau jamani...yule mwehu na mwehu haswa wanatuletea shida mbeleni
 
Tangia muda anaanza kujiroposha roposha kuhusu ukumbi kuchafuliwa na viongozi wa Yanga nikajua lazima atanogewa na kuharibu mambo.

Pole yake japo huwa namuona kama sikio la kufa ambalo saa nyingi linajali hisia za followers wake huko Insta.
ameharibu sana ule sio ujanja tena maana mhhh kusema wanayanga hamtakiwi dohh..aya ataenda pekeyake basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…