Simba kupata bao kwa Nkana sio shida, shida ni kuwazuia nao kupata bao

Wanasimba na Watanzania wazalendo,

Kesho Simba inawakilisha nchi kwenye mechi muhimu kabisa ya marudio. Kikosi cha sasa cha Simba inawezekana kuwa moja ya vikosi bora kabisa toka club hii ianzishwe labda ukitoa vikosi vichache kikiwemo kile kilichofika fainali kombe la CAF mwaka 93.

Ninaomba technical coach wa Simba amtumie stopa tegemeo wa Uganda Cranes Juuko Murshid kama beki wa kati akisaidiwa na Wawa huku Erasto Nyoni akicheza kama beki wa kulia.

Vile vile asiwatumie John Boko na Kagere kwa pamoja bali ni vema mmoja aanze ili timu iwe na wachezaji wengi wenye uwezo wa kuwapikia wafungaji.

Kocha ndiye mwenye maamuzi na ufahamu wa kutosha kuhusu wachezaji na mfumo anaotaka lakini na sisi mashabiki si mbaya tukiwashauri kwa jicho letu la jukwaani.

Kila lakheri mnyamaaaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…