Simba kupata bao kwa Nkana sio shida, shida ni kuwazuia nao kupata bao

Yule winga aliyefunga bao la 2 kule kitwe hawezi waacha salama, hata wamloge vipi mguuni kakwe ana goli2
 
Kupitia ukarasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook, uongozi wa Nkana FC umewaomba mashabiki wa Yanga kuisapoti timu hiyo katika kampeni yake ya kuiondoa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa kutokana na uwepo wa Kessy aliyewahi kutumikia timu yao.

Taarifa hiyo ilisema kuwa: “Wapendwa mashabiki wa Yanga acha kwa sasa tuwe familia ya Nkana Yanga, Nkana pia ni timu yenu, jiungeni pamoja nasi wikiendi hii Dar es Saalam kwa kuipa sapoti Nkana ili iweze kuwaondoa Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Lakini na mashabiki wa Yanga wakumbuke Kessy pia ni mtoto kutoka kwenye ardhi yao, wampe sapoti wikiendi hii,” ilisema taarifa hiyo.
 
Simba pale nyuma aanze wawa na juuko, alafu elasto aende beki wa kulia , shabarara kama kawa, kotei dimba la chini mkude juu, dilunga na chama, okwa na kagere, sub kichuya na boko, game tunashinda
 
dah timu za afrika mashariki zinaisha hahaha, yaani gormahia ilikua na faida ya goli mbili ila imetolewa

Kariobangi sharks nao wanafata kutoka

Tunabaki simba na kcca ya uganda, maana vipers nao walitoka mapema tu, tena kwa aibu

Dah masikini gormahia!! unashinda goli 3-1 nyumbani halafu ugenini unaruhusu 2-0

Dah poor Kenyans.
 
Simba pale nyuma aanze wawa na juuko, alafu elasto aende beki wa kulia , shabarara kama kawa, kotei dimba la chini mkude juu, dilunga na chama, okwa na kagere, sub kichuya na boko, game tunashinda
Tatizo kocha kamkariri boko
 
Hawahitaji kuomba. Support ipo kama kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…