SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Simba imeondoka leo kuelekea Morocco katika mtanange wa kufa na kupona dhidi ya Wydad AC. Katika safari hiyo, Captain wa Simba John Bocco ameachwa nyumbani. Hii ni safari ya pili mfululizo ambapo Bocco ameachwa katika safari wakati katika uwanja wa mazoezi anaonekana. Safari ya kwanza ilikuwa ile ya Botswana kucheza dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Kuna dalili zote kuwa Benchikha hakubaliani na uwepo au uongozi wa Bocco katika timu maana hizi ni mechi muhimu sana na kuachwa kwa Bocco katika safari nzima kuna tafsiri iliyo wazi.
Nani unadhani anastahili kuchukua unahodha wa Simba?
Kwa mtazamo wangu, Simba inahitaji nahodha mwenye ufahamu mzuri wa lugha ya kigeni, hii itasaidia kuwakabili marefa katiks mechi za kimataifa. Pia inabidi kuwa anaweza kuisimamia timu na kuhakikisha nidhamu na ari ya kushindana kupo kwa hali ya juu ndani na nje ya uwanja wa mazoezi na mechi.