Simba kupiga mechi mbili za kirafiki nchini Afrika Kusini

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Skwadi ya Simba ambacho kimepiga kambi nchini Afrika Kusini, ndani ya wiki hii kitaanza kucheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo.
Kikosi hicho ambacho kiliondoka nchini Jumatatu ya wiki iliyopita, kwa wiki nzima kimekuwa kikifanya mazoezi makali chini ya Kocha Mkuu Joseph Omog pamoja na msaidizi wake, Jackson Mayanja.

Simba ambayo itakuwa huko mpaka mwezi ujao, inatarajiwa kurejea nchini Agosti 6, mwaka huu kabla ya kufanyika kwa tamasha lao la Simba Day litakalofanyika Agosti 8, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Akizungumza kutoka Afrika Kusini, Mayanja alisema baada ya kufanya mazoezi ya nguvu kwa wiki nzima, wanatarajia wiki hii kuanza kucheza mechi za kirafiki bila ya kufafanua dhidi ya timu gani.

“Wiki ijayo (wiki hii) ndiyo tunatarajia kuanza kucheza mechi za kirafiki, mpaka sasa bado sijafahamu ni dhidi ya timu gani tutakazocheza nazo, lakini mipango ipo hivyo.

“Kikubwa ambacho naweza kusema, mazoezi yetu yanakwenda vizuri tukiwa na wachezaji wachache ambao hawakuwa na majukumu na timu zao za taifa, lakini muda wowote kuanzia sasa tunaweza kuwapokea wale waliokuwa Taifa Stars pamoja na wachezaji wapya,” alisema Mayanja

Kwa Hisani ya Salehe Jembe
 
Asante kwa taarifa mkuu..kila la heri kwa watani zangu
 
Ni mechi dhidi ya timu za daraja la nne huko south
 
Mbona habari za 7G ni za uzushi! Na nikwanini tuanze kuwatakia mabaya kabla hata hawajacheza mechi hata moja ya kirafiki? Watz wanachukia sana vya kwao isee.
 
Mechi ya kwanza kapigwa 7G

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kweli Simba siwapendi, lakini kwa hili la 7-0 ni uzushi. Tusubiri wacheze wakandamizwe tu kihalali.

Hata hivyo, huenda watacheza na timu za madaraja ya chini. Mamelodi Sundowns walikuja hapa Bongo mwaka jana, Simba na Yanga waligoma kucheza nao kwa madai kuwa walikuwa bize na ratiba zao. Nadhani huu ni muda muafaka wa timu za South Africa kulipa kisasi kwa kile tulichowafanyia Mamelodi Sundowns.
 
Hivi ile ya kupigwa7-0 ni ya kweli au uongo
 
Mbona habari za 7G ni za uzushi! Na nikwanini tuanze kuwatakia mabaya kabla hata hawajacheza mechi hata moja ya kirafiki? Watz wanachukia sana vya kwao isee.
Washabiki wa Yanga fc, wengi ni wambea. Wamezoea maisha ya udaku.

Wanakazania kutangaza goli saba hadi mishipa inawatoka utadhani walicheza wao huo mpira.
Dunia ya sasa ni kama kijiji huwezi kuficha kitu.
Hii yote ni hasira ya mazoea toka kuweka kambi Uturuki hadi kuweka kambi Kimbiji.
Msijali mwakani mtaenda kuweka kambi, Ufaransa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…