supermarket
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 7,453
- 10,952
Juzi pia Rage amepigilia msumari zaidi kuhusu hassan kessy.
Watani huwa hawana moyo kama wato.... Wao hupenda miteremko mno..... Ndio maana wamekuwa wakipata shida sana kunyanyua makwapa.....
Kwenye Kesi ya Hassan Kessy walikuwa wanashinda kwa waganga wakiomba YANGA ipokwe alama... [emoji23]
Ukisoma Comments zao hapa... Utagundua kuwa huwa hawapendi kanuni ziwavute shati... [emoji23]Wamesahau
Huko kwa Kessy kulikuwa na kanuni lakini eti hili halina kanuni. Maadam kuna ITC na leseni basi mambo ya work permit haiwahusu.
We have a long way to go!
Utazichukua kwa kanuni na sheria zipi? [emoji23]Tff wajaribu ujinga huo waone tunavyochukua pointi zte za yanga walizo mchezesha mchezaji wa simba hassan kesi
Swali zuri kwa uwezo wa akili yako.Pointi zinachukuliwa kwa kanuni na sheria. Kama kanuni hamna unampigia mbuzi gitaa.Utazichukua kwa kanuni na sheria zipi? [emoji23]
Mbona huko ulaya wachezaji hawaruhusiwi kucheza bila work permit? Tena hiki huwa kikwazo kikubwa!!!!
Kama unaongea kwa maslahi ya Simba, fikiri mara mbili; hoja yako inapingana na msimamo wa Simba hiyohiyo ilipokomalia uharamu wa Kessy kuiwakilisha Yanga kwenye Nane Bora za Kombe la CAF licha ya kwamba alikuwa na leseni ya CAF tayari! Mantiki ya hoja ya Simba ni kuwa leseni pekee haitoshi kumhalalisha mchezaji ikiwa taratibu nyengine hazijakamilika. Na ndio hoja anayojaribu kuijenga mtoa mada.Mfumo unaousema ni leseni ya kusajili haitolewi bila ya work permit. Ukishatoa leseni ni kwamba mchezaji yupo huru kucheza. Hamna kanuni itakayoweza kumzuia. Kama ipo itoe.
Falsafa ya kisheria ni kwamba Katiba (ya nchi) ndiyo Sheria Mama na kwa hivyo sheria yoyote inayopingana na Katiba ni batili. Kadhalika Sheria ndiyo mama wa kanuni na kwa hivyo kanuni yoyote inayopingana na sheria ni batili. Sheria ya ajira ni kwamba waajiriwa kutoka nchi nyengine ni lazima wawe na vibali vya kufanyia kazi nchini. Kwa hivyo wageni kufanya kazi bila ya kibali ni kukiuka kanuni yoyote iliyopo (hata kama kanuni yenyewe itakuwa imetoa uhalali au iko kimya kama hii ya Ligi) kwa kuwa inapingana na Sheria.Jibu rahisi la swali lako ni Ulaya kanuni hiyo ipo husajili mchezaji mpaka awe na work permit. Hapa Bongo tunakurupuka tu. Hamna kanuni hiyo kwenye sheria zinazosimamia mpira nchini.
Kuhusu kukatwa point Simba usahau mkuu. Cha kuwashukuru ndanda ni kuitoa TFF usingizini, naamini wataongezea hicho kipengele cha work permit kwenye kanuni zao. Ishu ya wachezaji kucheza bila work permit kilikuwepo tangu enzi za FAT! Mfano tu Ngandu Ramadhani alicheza kienyeji na akaondoka kienyeji kina Mwinyi Rajab, Masudi Shabaan hata Wasso hao ni kwa uchache tu!Tuseme Ndanda wamekurupuka hawajui kanuni hata kidogo
Kamati husika ije na majibu haraka kukata mzizi wa fitna
Acha kutumia akili ya mtoto mchanga kuandika.Kama unaongea kwa maslahi ya Simba, fikiri mara mbili; hoja yako inapingana na msimamo wa Simba hiyohiyo ilipokomalia uharamu wa Kessy kuiwakilisha Yanga kwenye Nane Bora za Kombe la CAF licha ya kwamba alikuwa na leseni ya CAF tayari! Mantiki ya hoja ya Simba ni kuwa leseni pekee haitoshi kumhalalisha mchezaji ikiwa taratibu nyengine hazijakamilika. Na ndio hoja anayojaribu kuijenga mtoa mada.
Itabidi TFF waje na hiyo kanuni. Vinginevyo wanashiriki kuikosesha nchi mapato!Kuhusu kukatwa point Simba usahau mkuu. Cha kuwashukuru ndanda ni kuitoa TFF usingizini, naamini wataongezea hicho kipengele cha work permit kwenye kanuni zao. Ishu ya wachezaji kucheza bila work permit kilikuwepo tangu enzi za FAT! Mfano tu Ngandu Ramadhani alicheza kienyeji na akaondoka kienyeji kina Mwinyi Rajab, Masudi Shabaan hata Wasso hao ni kwa uchache tu!
Hakuna kanuni hiyo mkuu. We subiri kukuche utatute supu unywe. Achana na hii habari, ishakwisha. Ndanda wamesaidia tu kuizindua tu TFF kuweka hicho kipengele. Na jana Afisa wa uhamiaji ametoa ushauri hicho kipengele kiwekwe ili kufisukuma vilabu kushughulikia mapema.Itabidi TFF waje na hiyo kanuni. Vinginevyo wanashiriki kuikosesha nchi mapato!
WASISAHAU KUIPOKA YANGA POINT 24 WALIZOMCHEZESHA KESSY DURU LA KWA LIGI KUU!
BY 13BILLIONS PSPF
Vipi mmeshapewa pointi 3?Mliambiwa hamna kanuni hiyo hamsikii. Mmeanza kupiga wachezaji sasa?Itabidi TFF waje na hiyo kanuni. Vinginevyo wanashiriki kuikosesha nchi mapato!