Ngoja basi hata mechi 10 zipitie mkuu ndio uhitimishe mmepigwa.Kiufupi hakuna neno lingine la kusema kwa Mutale zaidi ya simba tumepigwa hakuna mchezaji hapo.
Tumemuondoa Saido tumeleta Saido namba mbili ( Mutale) mbovu zaidi ya mara 10 ya Saido namba 1.
Bora Ntibazonkiza alikuwa ana faida kwenye mipira iliyo kufa lakini Joshua Mutale hana faida yeyote zaidi kukimbia kimbia hovyo na kuwa mzigo kwa wachezaji wenzake uwanjani.
Usimkatie mtu tamaa mapema hivyo.Hakuna mchezaji hapo aina ya uchezaji wake inamhukumu , yaani ana mambo mengi sana yasiyo kuwa na faida yeyote uwanjani.