Simba kwenye uumbwaji

Mingendeu

Senior Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
115
Reaction score
237
Hapo mwanzo Simba haikuonekana timu tishio. Kila mshabiki wa Simba hakuwa na tumaini na timu yake. Ndipo Mo akasema, anarudi kwenye uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi. Ikiwa jioni, ikawa asubuhi siku ya kwanza.

Mo akamleta Camara akasaidiane na Manula, Salim na Abel. Mo akamwambia Camara, kwa muda mrefu tulihitaji kipa anayeweza kucheza ili tuanze kujenga mashambulizi kuanzia nyuma. Camara akasimama kwenye milingoti 3.

Akaenda kuifanya kazi vyema kama alivyoagizwa. Mpira aliucheza na kudaka alidaka. Ubora mkubwa wa Diara kwa misimu kadhaa. Umepata mshindani wa kweli. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

Mo akamuita Chemalone, akamwambia nikuletee nani? Chemalone akasema , niletee Karabou. Mo akamuongezea na Hamza. Kisha akawaambia.

Simba ni timu inayopenda kucheza mpira. Nendeni mkatuletee burudani uwanjani. Mzuie lakini pia mcheze, mburudishe washabiki na kuelimisha mabeki wengine wa Tanzania. Nao wakafanya kama walivyoagizwa. Ikawa jioni, ikiwa asubuhi siku ya tatu.

Mo akawasikiliza watanzania, washabiki wa Simba kwa wachambuzi, Kuwa Mohammed Hussein na Kapombe wamechoka, Watafutiwe mbadala. Duchu akarudishwa kundini, Kijili na Valentino Nouma wakaletwa ili kuwapumzisha wakongwe.

Ujio wa Kijili ukawa catalyst kwa Kapombe, na timu ya taifa akarudi. Kule kwa Zimbwe kazi ipo. Akicheza yeyote hakuna tatizo. Ikiwa jioni, ikawa asubuhi siku ya nne.

Mo akamleta Mavambo na Okejepha, wakatawale kiungo. Dimba la juu na la chini likawekwa himayani kwao, kisha akawaongezea Kagoma, Akamwambia, nenda katukumbushe kile kiungo cha Kotei.

Mzamiru akaambiwa, atulie awape wenzake uzoefu, Ngoma akapewa jukumu la kuwa nahodha msaidizi, akaambiwa apige pasi elekezi, na urefu wake akasaidie kufunga mipira ya adhabu na kona.

Nao wakatingisha kichwa kuonesha wameelewa maelekezo, wakaenda kuitenda kazi kama walivyoagizwa.
Ikawa jioni, ikawa asubuhi siku ya tano.

Mo akamleta Barua, Chasambi na Mutale, Ahoua na Awesu. Wakaongeza machachali pembeni ya uwanja na katikati. Magoli yakapatikana. Ikiwa anaelekea kupumzika akawaletea Fadlu kuwa Mwalimu.

Fadlu akasema 'timu inajengwa' sio ya 'kuchukua ubingwa'. Watu wakawa hawamuelewi kwa kauli zake maana timu inayojengwa ndiyo ikaongoza msimamo wa ligi.

Timu inayojengwa inapata matokeo kwenye mashindano ya kimataifa. Ikaacha maswali , Ikiwa timu bado inajengwa ndio matokeo haya? Je! baada ya ujenzi itakuwaje?

Ikawa jioni, Ikawa asubuhi siku ya sita.

Siku ya Saba Mo akiwa amepumzika. Ndipo akakutana na andiko, Je ni nani atakayeacha kondoo wake asinywe maji siku ya sabato?

Mo akainuka na kumuuliza Fadlu, Mwalimu nikuongezee nani? Fadlu akasema sio vyema Mukwala awe peke yake. Mo akamleta Valentino Mashaka na Ateba kuwa wasaidizi. Kisha wakamuongeza na Mpanzu.

Point tatu zinapatikana na timu inacheza. Kocha anasema bado anaijenga timu, boss anauliza nimlete nani?

Kwa maelezo ya Fadlu bado timu ipo kwenye uumbaji. Ijapokuwa timu inakusanya point 3. Baada y uumbaji. Tutegemee makubwa zaidi.
 
Simba bado inahitaji marekebisho makubwa.

1. Ayoub Rakred.
2. Karabou Chamoe.
3. Okejepha.
4. Joshua Mutale.
5 .Mukwala.
6. Nouma.

Wafanye swap ya Msindo na valentine Nouma.
 
Ila liCamara linatuokoa aisee. Kuna mikiki inapigwa anaitoa mpaka unashangaa
Ni aina ya Kipa aliyehitajika Simba kwa muda mrefu. Na kila siku zinavyoenda anazid kuwa bora. Amepunguza Sana Kufanya makosa. Kwenye ubora wake, wapongezwe pia mashabiki wa Simba kwa kutompa pressure kubwa baada ya makosa kadhaa kwenye mechi ya Yanga na ile ya Coast
 
Mzee unakitu ktk kuandika🤝🤝
 
Simba bado inahitaji marekebisho makubwa.

1. Ayoub Rakred.
2. Karabou Chamoe.
3. Okejepha.
4. Joshua Mutale.
5 .Mukwala.
6. Nouma.

Wafanye swap ya Msindo na valentine Nouma.
Nouma na Karabou wameshaonesha bado wanahitajika Sana. Mukwala pia sidhani Kama ni mchezaji mbovu. Nahisi Simba inahitaji kiungo wa aina ya Chama. Kiungo wa namna hii ndiye anayekosekana na ni adimu Sana hawa sokoni
 
Nikikumbuka ule mtobo wa Nzengeli alompiga Camara wenu nacheka😂🤣
 
Nouma na Karabou wameshaonesha bado wanahitajika Sana. Mukwala pia sidhani Kama ni mchezaji mbovu. Nahisi Simba inahitaji kiungo wa aina ya Chama. Kiungo wa namna hii ndiye anayekosekana na ni adimu Sana hawa sokoni

JIFUNZE KWANGU DOGO NENO LANGU KWENYE MPIRA NI SHERIA.

SIMBA INA SHIDA KWENYE.
BEKI 5.
KIUNGO 6.
KIUNGO 10.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…