Tetesi: Simba meza moja na kocha wa zamani wa Mamelodi

Tetesi: Simba meza moja na kocha wa zamani wa Mamelodi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Klabu ya Simba imeripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na aliyewahi kuwa kocha wa Mamelodi Sundowns, Steve Komphela ambaye hivi sasa yupo jijini Dar Es Salaam

Simba Sc ambayo imekuwa chini ya Mtanzania Juma Mgunda kwa muda inatafuta kocha mpya kwa ajili ya kampeni za msimu ujao.

Aidha zipo ripoti kuwa Juma Mgunda ameruhusiwa kuondoka klabuni hapo kwa ajili ya kwenda kukinoa kikosi cha Coastal Union.
 
Mgunda Simba wanamsumbua lakini mladi pesa inaingia mfukoni
 
Ila Simba vichekesho Sana.

Yanga ilipomuajir mwarabu Nabi Simba wakaona wamuajir muarabu Benchikha

Yanga walipomuajir Kocha wa Zamani wa Mamelod Gamond nao Simba wameenda Kwa huyo Kocha wa Zamani wa Mamelod

Yanga waliposajil wachezaj Asec Simba wakaona wasibak nyuma wakamkwapua Kramo.
 
Ni kweli vilabu vyetu Simba na Yanga hawa wafadhili wanajipigia watakavyo ila kwa sasa Simba imezidi usanii.
 
Hivi huyu mbona Huwa hatusikii timu za nje zikimtafuta pamoja na masifa mnayompa?

Embu acheni viongozi wa timu wafanye kazi Yao!
Huwa tunashangaa makocha wakitimuliwa yeye huwa timu inafanya vizuri zaidi
 
Uongozi wa Simba unafurahisha sana. Kila mwaka wanaajiri kocha, na timu ikiyumba kidogo tu wanamtimua na kuwaweka makocha wao wa muda. Kama siyo Selemani Matola, basi ni Juma Mgunda.
 
Back
Top Bottom