Simba mkazo uwe kujenga wachezaji kisaikolojia ili kushinda lubumbashi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Siku kadhaa zilizopita ulitembea waraka kwenye mitandao ya kijamii kuwa huenda simba ikatolewa kwa sababu inatumia madawa.

bila shaka yoyote itakuwa timu pinzani inayoshindana na simba ndio waliobuni waraka huo ili kunyongonyeza morali ya wachezaji.

wapo waliosoma waraka ule wakabaki na mashaka kuwa hivi haya madai yanaweza kuwa ya kweli?

mashaka haya lazima yalikuwa hata miongoni mwa wachezaji ambao yawezekana vichwani mwao walijiuliza hivi hizi tuhuma ni kweli au za uongo?

kwa wachezaji kushinda mechi kadhaa na kuingia hatua ya juu ni kitu kinachowajenga molari ya kutafuta mafanikio zaidi. Lakini pale mtu anapoingiwa mashaka kuwa pengine mafanikio yake hayakutokana na juhudi zake basi mtu huyo ataacha kutilia mkazo juhudi.

Mbinu inayotumiwa na timu pinzani ni kutumia kila mbinu, kutumia mpira uwanjani, kucheza na saikolojia za wadau pinzani n.k

Simba uwezo wa kucheza mpira mnao hivyo jiandaeni kukabiliana na timu pinzani katika nyanja zote.

jengeni wachezaji wenu kuwa ukitazama uwanja ukaona jezi za timu pinzani wakishangilia wakati wote wewe weka nia ya kumuadhiri mpinzani wako mbele ya wapambe wake, kadiri wanavyoshangilia ndivyo nyinyi mnavyokomaa zaidi.

hapa tafuteni vitu sensational ambavyo watu au jamii inaonekana kuadhiriwa mbele ya jamii zao zilizokuwa zikiwasapoti alafu mgeni anapomwadhiri mwenyeji, watu kimya na mgeni anapita katikati hana hata wa kumshangilia bali kupigwa na butwaa. Jenga fikra zao kwenda kufanya haya

Tafute matokeo mnayohitaji, kama ni ushindi na ushindi ukikosekana na kutambua pengine suluhu ya mabao inaweza kutubeba. hivyo ni kuwajenga wachezaji wasiruhu kufungwa, ikitokea wamefungwa lazima wa react haraka kutafuta kusawazisha wakijua tukisawazisha tunapita kwa goli la ugenini

kama mnaweza kutumia mitandao kuwatengenezea na wenzenu propaganda ili ziwachanganye. mfano mwamuzi kabadailishwa ni fursa ya kutumia watu wasio rasmi kutengeneza panic kwenye kambi ya adui. anaweza kutokea muhuni akatengeneza taarifa kwenye mitandao yao kuwa jamaa wamekamatwa wakitoa mlungura hivyo watatolewa.

Tafuteni historia fupi fupi za timu zilizopindua matokeo ugenini mfano Man U Vs Psg, tafuta mechi kadhaa, waeleze wachezaji mkirudia rudia haya yawakae kichwani. leo unawaambia timu hii, kesho unakuja na stori tofauti ya timu nyingine iliyofanya maajabu kesho kutwa unaibuka na stori nyingine na zote ziwe real na kusisitiza kupata matokeo ugenini inawezekana ni, focus,

mengine mjiongeze sisi watz tunachotaka ni matokeo chanya
 
kwa record ya simba ugenini, kazi ipo,maana mazembe wakiwa kwao ni habari nyngne, mi mshabiki wa yanga ushauri wangu kwa hawa mikia ni kuwa japokuwa wako vzuri sn ila ili kuendelea kufny vzuri kwe CAF msimu ujao watagute striker mwenye uwezo mkubwa ambae atateam na kagere na okwi, apatikane beki wa kushoto mwny uwezo mkubwa km beki wao wa kuliab yule then waongeze kiungo mmoja mkali km chama itakua poa sana, ila pia km yanga na azam zitaendelea kuwa dhaifu basi simba itaathirika sana kutokana na kucheza ligi dhaifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…